Wazazi na jamaa wa wasichana wa
shule waliopotea nchini Nigeria baada ya kutekwa nyara wamewaomba
wapiganaji wa kiislamu kuwa na huruma na kuwasihi kuwaachilia watoto wao
.
Mkuu wa shule yao anasema zaidi ya wasichana mia moja na nane bado hawajulikana walipo.Wachache walibahatika kutoroka , lakini mkuu wa shule hiyo anasema wasichana mia moja na nane bado hawajulikani walipo .
Mmoja wa baba wasichana hao amesema kuwa anatumai serikali itafanya mazungumzo na wapiganaji hao wa kiislamu , kwa sababu anasema anahofu kuwa matumizi ya nguvu itawaweka hatarini zaidi wasichana .
Amewaomba Boko Haram kuonyesha huruma.
La kushangaza ni kwamba maafisa wa Nigeria wamekaa kimya kuhusiana na utekaji nyara huu.
Rais Goodluck Jonathan hajatoa tamko lolote kuhusiana na tukio hili . Jeshi linasema linajaribu kuwanusuru wasichana hao , lakini haifahamiki juhudi hizo zimefikia wapi.
0 comments:
Post a Comment