Makamu wa Rais wa Marekani Joe
Biden amesema sharti Urusi ikome kuongea sana na badala yake ianze
kufanya kazi ya kusitisha mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine.
Bwana Biden aliyasema hayo wakati wa mkutano na
waandishi wa habari ambapo waziri mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk pia
alihudhuria. Joe Biden, amesema kuwa Marekani iko tayari kuwasaidia viongozi wa Ukraine kufikia kile alichokitaja kuwa fursa ya kihistoria ya kujenga taifa la Ukraine lenye umoja.
Biden pia aliwahutubia wabunge mjini Kiev katika ziara iliyopangwa kuonyesha uungwaji mkono wa Marekani kwa serikali ya mpito ya Ukraine.
Bwana Biden amesema kuwa uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi ujao ni muhimu zaidi katika historia ya taifa hilo.
Wakati huohuo Biden amesema kuwa Marekani haitawai kutambua alichosema ni Udhibiti haramu wa jimbo la Crimea ambalo linadhibitiwa na Urusi.
Amesisitiza kuwa Ukraine ni nchi moja na inapaswa kusalia hivyo.
Amesihi Urusi,kuhakikisha kuwa mkataba uliofikiwa wiki jana wa kusitisha mgogoro kwa kuamuru vikosi vya Ukraine vinayounga mkono Urusi nchini humo kuondoka katika majengo ya serikali waliyoyateka Mashariki mwa Ukraine.
Kadhalika Biden alisema kuwa pamoja na msaada zaidi wa dola bilioni 50 unaodhamiria kusaidia kuchepua uchumi na kuleta mageuzi ya kisiasa,Marekani pia inaahidi kutoa msaada wa kijeshi.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali za kimataifa kwa wakati muafaka...................
0 comments:
Post a Comment