Matangazo hayo yaliyokuwa yanarushwa na TBC1
wakati Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya walio wachache katika Kamati
Namba 4, yalikatishwa ghafla na kumlazimu mwenyekiti wa Bunge, Samuel
Sitta kuahirisha kikao hadi leo.
Wakati Zitto akipendekeza kufanyika kwa uchunguzi
huo, Baraza la Habari Tanzania (MCT) limetaka kuwapo uthibitisho wa
kitaalamu uliosababisha kukatika kwa matangazo hayo.

Hata hivyo, meneja matukio wa TBC, Mbwilo Kitujime alisema kwa ufupi kuwa hakukuwa na siasa katika suala hilo bali mitambo ilipata hitilafu, lakini akasema kwa ufafanuzi zaidi atafutwe mkurugenzi mkuu wa TBC, Clement Mshana. Mshana hakuweza kupatikana.
Kauli ya Zitto
Akizunguza kwa simu kutoka nchini
India jana, Zitto alisema sababu nyepesi tu kuwa “ni kutokana na hali ya
hewa Dar es Salaam” hazikubaliki, hasa kutokana na mwenendo wa TBC.
“TBC inaendeshwa kwa fedha za walipa kodi. TBC
ijue kuwa wao si shirika la utangazaji la serikali, bali ni Shirika la
Umma. Ni matumizi mabaya ya fedha za umma kuegemea upande mmoja,”
alisema.
Zitto, ambaye pia mbunge wa Kigoma Kaskazini na
mjumbe wa Bunge hilo, alipendekeza shughuli za TBC kipindi hiki chote
cha mjadala wa Katiba ziwekwe chini ya uangalizi wa chombo huru chenye
wajumbe kutoka pande zote.
MCT yahoji mfumo
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alisema
mfumo wa sasa wa uendeshaji wa shirika hilo la umma ni mbovu na una
kasoro na ndio maana wadau wa habari walipendekeza mabadiliko makubwa
katika shirika hilo.
“Kitu kilichotokea jana (juzi) kinathibitisha
mambo ambayo tumekuwa tukidai kwamba tutoke kwenye kitu kinachoitwa
utangazaji wa serikali twende kwenye utangazaji wa huduma za umma,”
alisema.
Kwa mujibu wa Mukajanga, TBC inapaswa kujiendesha
kama lilivyo Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), ambalo ni huru
likiwa na kasma maalumu na linawajibika moja kwa moja kwa Bunge.
0 comments:
Post a Comment