Facebook

Monday, 1 September 2014

Diamond avamiwa wakati akiwa jukwaani Ujeruman.

Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira
ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa
Bongo Flavor, Nasib.   Abdul maarufu kama
Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya
hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini
Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki
waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.

Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na
washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.
Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi
euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show
ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta
wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo
mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani
na promota wake raia wa Nigeria anayejiita
Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa
hawakutendewa haki walianza kurusha chupa
na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond
na promota wake, Kilichowakera zaidi
washabiki ni pamoja na vyombo vibovu
vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu
ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja hadi
vyombo vya muziki, ma-Djs walishambuliwa
na wapo hospitalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake,
mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa
moyo na kukimbizwa hospitali, washabiki hao
walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi
hospitali.

Polisi nchini Ujerumani
wanamesema tukio hili la aibu halijawahi
kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika
jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari
kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu
sana muda wao.
Diamond Platnumz akiwapagawisha
mashabiki wake katika moja ya maonyesho
yake.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa
onyesho hilo na wamesema wanachunguza
thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia
hizo na pia itamfungulia mashataka promota
huyo raia wa Nigeria ambaye pia
anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao
fulani wa biashara.

0 comments:

Post a Comment