Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday, 29 November 2014

Kafulila: Nilikuelewa vizuri sana ulipo tofautiana na Mtoto wa Mgimwa.

Kwanza tuhuma alizozitoa J.J.Mnyika zilikuwa na mashiko sana, kwamba kifo cha Mgimwa kina utata na kinatakiwa kichunguzwe na serikali. Kwanza ilianzia kwa Zitto Kabwe kusema wazi kuwa mama yake aachwe apumzike, Zito nilimwelewa, baada ya hapo mtoto wa Mgimwa naye ataomba Baba yake aachwe apumzike na asihusishwe na sakata la Tegeta Escrow Account kwa namna yoyote ile.

David Kafulila kwa nini nasema nilimwelewa vizuri: Alileta hoja kuwa Mgimwa alikuwa kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tena katika ngazi ya juu kabisa. Kwa hiyo hoja ya Uchunguzi wa kifo chake ni wazi kabisa kama alivyonena Kafulila.

Mtoto wa Mgimwa yeye anamtetea Baba yake, lakini Taifa linataka kuchunguza kifo cha Kiongozi na si Baba wa Mtu fulani. Ni kama Rais wa nchi auwawe afu mtoto wake aseme sitaki Uchunguzi wa Baba yangu kwani hata mkifanya hawezi kurudi!!!!. Kiongozi mkubwa wa nchi si Mali ya familia jamani, akiwa nyumbani kwake ndiyo Baba yenu na akiwa nje atabaki kuwa kiongozi wa Taifa, na hata akifia nyumbani kama kifo ni cha utata lazima serikali ifanye Uchunguzi tu.

TAZAMA TYGA ALIVYOSHEREKEA THANKSGIVING DAY JANA

Ni kama miezi minne imepita tangu zilipotokea tetesi za kuwa Tyga anatoka na Kylie Jenner aliye na miaka 16,mdogo wake Kim Kardashian West.Tyga alimualika Kylie katika sherehe ya Thanksgiving Day ambapo Kylie hakuwa na wasiwasi wowote alipoonekana akipiga story na Chris Brown na marafiki wengine.
Tyga alionekana na mtoto wake Cairo mwenye miaka miwili,bila ya mama yake Black Chyna.Siku mbili kabla walionekana pamoja wakicheka na kufurahi katika event ya  Los Angeles Mission. 





WIZ KHALIFA NAYE AJARIBU KUBREAK INTERNET,,LOL!!

Rapper Wiz Khalifa aliwashangaza mashabiki wake pale alipopost picha akaijaribu naye eti kubreak internet kama Kim Kardashian alivyofanya wiki kadhaa zilizopita.Picha hiyo iliyomwonesha akiwa uchi bafuni na kuiweka kwenye Instagram.Alionekana akiwa anajimwagia maji kutoka kwenye chupa kutumia mkono mmoja huku mwingine ukiwa umeshikilia sehemu zake za siri.Aliweka caption " No shower til 4pm."
Story by Samchris Swai

Friday, 28 November 2014

Tibaijuka "Nilipokea pesa za ESCROW"

Mjadala kuhusu kashfa ya uchotaji wa
mamilioni ya fedha katika akaunti ya ESCROW
ya Benki Kuu ya Tanzania umezidi kuunguruma
nchini Tanzania kufuatia taarifa ya Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC,
na ripoti ya serikali kuhusu kashafa hiyo.
Mambo yaliyojitokeza katika ripoti ya PAC ni
kutaja majina ya viongozi na maafisa
wandamizi wa serikali walionufaika na magao
huo.

Miongoni mwao ni waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
ambaye alizungumza na mwandishi wetu mjini
Dodoma, Ben Mwang'onda ambaye alianza kwa
kumuuliza kama kutajwa kwa jina lake
alitendewa haki

LIVE:-Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Ijumaa, Tarehe 28 Novemba, 2014

 
Habari wakuu,

Leo tunamaliza ngwe yetu ya mwisho bungeni, baada ya wasilisho la ripoti ya PAC, majibu ya serikali na mjadala wa wabunge wa jana, moja kwa moja kutoka Dodoma tuwe pamoja kuimaliza ngwe yetu. TANESCO wameshatoa tangazo rasmi la matatizo ya umeme hivyo chaji zetu ziwe vizuri nafasi ya kupata umeme inapopatikana.
=============

SAA 3:00 ASUBUHI.
 
Spika ana Makinda ndiye aliekalia kiti leo na Mwanri anajibu maswali yanayohusu wizara ya afya.

MangungoNyongeza: Eneo la Mlandizi ni eneo la barabara kuu, nini ahadi serikali kuharakisha upatikanaji wa kituo ili kuwapelekea wananchi huduma karibu? Lipo tatizo la wahudumu wa afya na madaktari japo majengo yapo, nini jitihada ya serikali?

Mwanri: Nakubaliana eneo la barabarani ajali nyingi, tutajitahidi kukamilisha haraka na kuona inafanyiwa kazi. Kuna vibali vimetoka kwa wahudumu wa afya pia wizara pia inapeleka watumishi moja kwa moja.

Tuliwapa nafasi cha watumishi 8,000 wizara ya afya pia tumewapa kibali cha watumishi 1,000 na bado hakijamaliza.

Suzan Lymo: Maslahi ya walimu lazima yaboreshe, serikali inafahamu tatizo
Mwanri: Nakubaliana lazima kuboresha maslahi ya walimu, tuna upungufu wa walimu na nyumba za walimu. Mkakati wa serikali na pamoja na kudahili walimu na maabara, nyumba za walimu na kuimarisha mfumo wa kuwahudumia walimu.

3:25 ASUBUHI
Suzan Lymo: Kuna tatizo la upangaji walimu kwa shule za pembezoni, pia watendaji wanakaimisha walimu majukumu badala ya kukaa kwenye vituo vyao vya shule
Mwanri: Kwanza kweli kuna tatizo, lakini tatizo kwa walimu wa sanaa limpembukua sana, tutafanya upangaji(re-allocation). Mwalimu kazi yake ni kufundisha hivyo kuwapa kazi za watendaji haikubaliki.

Leizer: Ni lini serikali itachukua mkakati kwa nyumba za walimu kama walivyofanya maabara!
Mwanri: Jitihada za maabara tunazipongeza halmashauri, kuna halmashauri tumewapelekea milioni 500 kila moja ambazo zipo katika mazingira magumu.



SAA 3:45 ASUBUHI.





 
Maswali sasa ni kwa Wizara ya Nishati na Madini, ambapo maswali yanajibiwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe Stephen Masele.

Mhe Mbilinyi: Tunazaungumzia sana mafanikio ya kusambaza umeme, kuna umuhimu gani wa kuendelea kusambaza umeme wakati huwa unakatwa kwenye nyakati maalum. Mfano; Jana kwenye mjadala wa umeme?

Jibu: Tutofautishe kati ya kuwapatia umeme wananchi na kupatikana umeme wakati wote. Jana kulikuwa na hitilafu ndogo tu, ila Leo mbona umeme upo.

Komba: Katika Maeneo ya Mbamba bay, kwanini umeme mpaka sasa haujafika kama ilivyoahidiwa?

Jibu: Kuna Matatizo ya nguzo, kutokana na demand kuwa kubwa sana wakandarasi wameagiza nguzo za kutosha ili kuhakikisha miradi yote inakamilika.



SAA 4:00 ASUBUHI.

Maswali kwa wizara hii bado yanaendelea....

============================== =========

Sasa ni zamu ya maswali kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi.

Swali: Ni lini serikali itaboresha magereza kwa kuwa yapo kwenye hali mbaya kwa uchakavu, pamoja na miundombinu yake mibovu?

Jibu (Naibu waziri) : Serikali kupitia wizara yangu, ipo kwenye mikakati ya kutatua changamoto hiyo. 



SAA 4:05 ASUBUHI

Swali: Hivi karibuni, nchi jirani ya Kenya tukio la westgate lilitishia usalama wa nchi na raia wake, Je serikali imejipanga vipi kuzuia tukio kama lile lisiikumbe Tanzania?

Jibu: Tukio la Westgate la Kenya, lilikuwa ni tukio la kupangwa kwa masuala ya ugaidi. Serikali ya Tanzania kupitia jeshi la polisi, linajitahidi kwa makusudi kukusanya taarifa za kiintelijensia na kuimarisha ulinzi. 


SAA 4:20

 
==================

Maswali kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia


Swali: Ni kiasi gani makampuni ya simu za mikononi zimelipa Kodi kwa Mwaka uliopita?

Jibu: Makampuni ya simu hulipa kodi kwa utaratibu uliowekwa. Aina za kodi ni pamoja na VAT, Service, Corporate TAX na nyinginezo.

Swali Nyongeza:
Hivi karibuni serikali imeweka mtambo wa kudhibiti simu zinazoingia na kutoka nchini. Je, imeongeza vipi kodi (pato)?

Jibu: Ni kweli serikali imeweka mtambo wa mawasiliano pale TCRA, Mtambo huo una kazi zake mbali mbali. Lakini kwa sasa serikali imefikiria namna ya kupata solution ya kuangalia namna gani itakagua mobile money transfer ili kuweza kutoza kodi.

Swali nyongeza (Zungu): Mheshimiwa waziri hujatoa majibu ya kitaalamu, kwani mtambo huo bado kabisa haujaanza kufanya kazi kama inavyotakiwa kufanya. Sasa nauliza, ni lini software hii ya kutoza wafanya biashara hasa wa mitandao ya simu italetwa na kuanza kufanya kazi ili mwananchi ajue kodi yake inaenda serikalini moja kwa moja?

Jibu: Kwa sasa mtambo unafanya kazi ya kukagua simu zinazoingia na kutoka, za kihalifu pamoja na kukagua mawasiliano kwa ujumla. ILa Tunaamini mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu kazi hiyo itakuwa imekamilika.

ASKOFU KILAINI AKIRI KUPOKEA MILIONI 80.5.



 

Askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba Methodius Kilaini amekiri kupokea milioni 80.5 kutoka kwa James Rugemalira na akisema hii si mara yake ya kwanza kupokea fedha toka kwa mfanyabiashara huyo kwakuwa mara nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamiii. Na michango amesema michango inayopelekwa kwake haina siri hivyo washikwe wezi halisi sio yeye

Zitto kufanya majumuisho ya kamati ya PAC leo hii jioni na kujibu hoja inayomkabili.

 Zitto Kabwe

Hiki ndicho alichoandika kupitia ukurasa wake wa facebook
 
Leo jioni kuanzia saa Kumi na Moja nitafanya majumuisho ya hoja ya Kamati ya PAC kuhusu akaunti ya Escrow na uhalali wa Kampuni ya PAP kumiliki IPTL. PAC itajibu hoja za Serikali na Mimi kama Mbunge Binafsi nitajibu hoja dhidi yangu.

BantuTz MAGAZINE-Soma kilichoandikwa katika Magazeti ya leo Novemba 28.

.
BantuTz MAGAZETI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa katika kurasa za mbele na nyuma magazeti yote ya leo.
;
;
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC06195
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Endelea kufurahia huduma za BantuTz.com huku ukiusubiria kwa hamu Mtandao wa kijamii mkubwa na wa kisasa zaidi uitwao Bantuz hapo mwakani.