Kwanza tuhuma alizozitoa J.J.Mnyika zilikuwa na mashiko sana, kwamba kifo cha Mgimwa kina utata na kinatakiwa kichunguzwe na serikali. Kwanza ilianzia kwa Zitto Kabwe kusema wazi kuwa mama yake aachwe apumzike, Zito nilimwelewa, baada ya hapo mtoto wa Mgimwa naye ataomba Baba yake aachwe apumzike na asihusishwe na sakata la Tegeta Escrow Account kwa namna yoyote ile.

David Kafulila kwa nini nasema nilimwelewa vizuri: Alileta hoja kuwa Mgimwa alikuwa kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tena katika ngazi ya juu kabisa. Kwa hiyo hoja ya Uchunguzi wa kifo chake ni wazi kabisa kama alivyonena Kafulila.

Mtoto wa Mgimwa yeye anamtetea Baba yake, lakini Taifa linataka kuchunguza kifo cha Kiongozi na si Baba wa Mtu fulani. Ni kama Rais wa nchi auwawe afu mtoto wake aseme sitaki Uchunguzi wa Baba yangu kwani hata mkifanya hawezi kurudi!!!!. Kiongozi mkubwa wa nchi si Mali ya familia jamani, akiwa nyumbani kwake ndiyo Baba yenu na akiwa nje atabaki kuwa kiongozi wa Taifa, na hata akifia nyumbani kama kifo ni cha utata lazima serikali ifanye Uchunguzi tu.