Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Thursday, 17 September 2015

Bondia Manny Pacquiao atia neno baada ya Mayweather kutangaza kustaafu.

Bondia Manny Pacquiao amesema kwamba ameachana na ndoto za pambano la marudiano na Floyd Mayweather kutokana na mpinzani wake huyo kutangaza kustaafu kufuatia kumshinda kwa pointi Andre Berto mwishoni mwa wiki.

Mayweather alimshinda kwa pointi Pacquiao Mei mwaka huu katika pamabano la utajiri mkubwa wa ndondi na baada ya kumshinda Berto katika pambano lake la 49 mfululizo kushinda, ametangaza kustaafu akiwa hajapoteza pambano.

Hata hivyo, mashabiki walikuwa wanataka kuona akirudiana na Pacquiao kwa sababu katika pambano baina yao, Mfilipino huyo alipigana akiwa ana maumivu ya bega na pia hivi karibuni imeripotiwa Mayweather alitumia dawa zilizopigwa marufuku mchezoni. Pac Man anatarajiwa kuwa fiti kurejea ulingoni mwakani baada ya kupona bega.

“Ngumi si kitu nachofikiria kwa sababu naweza kupigana mwakani tu, ili kulipa mapumziko bega langu,”amesema Pacquiao leo ambaye anaendelea na matibabu ya bega lake la kulia aliloumia mazoezini kujiandaa na pambano dhidi ya Mayweather.
Mbabe huyo ambaye pia ni mwanasiasa nchini kwao, amesema kwa sasa ameelekeza nguvu zake katika ujenzi wa nyumba za watu wasio na makazi kusini mwa nyumbani kwao, jimbo la Sarangani.

“Niko sawa. Kuwe na pambano la pili (dhidi ya Mayweather), si tatizo,” amesema. “Nimesikia amestaafu, haijalishi,”. Kwa pambano lijalo, amesema atapigana na bondia yeyote. “Kwa sababu sichagui wapinzani wangu,”.
Pacquiao pia amesema alikuwa anasubiri kuona Mamlaka za ndondi Marekani zitamchukulia hatua gani Mayweather kwa kutumia sindano ya dawa za IV baada ya kupima uzito kabla ya pambano lao mjini Las Vegas.

UEFA kuanzisha mashindano mengine makubwa barani Ulaya.

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA huenda likafanya maamuzi ya kuandaa michuano mingine itakayohusisha vilabu vya nchi wanachama tofauti na ligi ya mabingwa barani Ulaya pamoja na Europa league.

Taarifa za ndani ya shirikisho hilo zinadai kwamba, tayari wazo wa kuanzishwa kwa michuano hiyo limeshawasilishwa kwa wajumbe wa kamati ya utendaji na wakati wowote litaanza kufanyiwa kazi.

Nchi wanachama wa UEFA ambao wapo 54, wameshakubaliana kwa pamoja juu ya kuanzishwa kwa michuano hiyo, na sasa wanasubiri kama wazo lao litapitishwa na kamati ya utendaji ya shirikisho hilo, kabla ya kurejeshwa kwao na kupigiwa kura ya ndio ama hapana.

Michuano hiyo inayopigiwa upatu kuanzishwa na UEFA itatoa nafasi ya kushirikisha klabu ambazo zitakua zinakosa nafasi ya kuendelea kwenye michuano ya Europa League ambayo huchezwa katika hatua tatu tofauti.

Pendekezo lililopo kwa sasa ni kuona michuano hiyo inaanza kuchukua nafasi yake barani humo kuanzia mwaka 2018.
Mtendaji mkuu wa shirikisho la soka nchini Ukraine, Volodymyr Geninson, amezungumza na vyombo vya habari na kusema anaamini wazo hilo litapatiwa baraka na uongozi wa juu wa UEFA na litaanza kufanyiwa kazi kwa vitendo.

Amesema lengo kubwa ni kutaka kuona klabu za soka barani Ulaya zinapata wigo mkubwa wa kushindana hata kama zitakua zimeshindwa kuendelea kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya pamoja na Europa League.

Kutolewa kwa wazo hilo, kunaendelea kuonyesha ni vipi shirikisho la soka barani Ulaya linavyojipanga kulisaidia soka la barani humo kwa kubuni michuano mbalimbali ambayo itashirikisha washiriki wengi kwa wakati mmoja.

Kama itakumbukwa vyema, tayari rais wa UEFA Michel Platini ameshaungwa mkono katika wazo lake la kutaka timu shiriki kwenye fainali za mataifa ya barani Ulaya kuongezwa na kuanzia mwaka 2016 mpango huo utaanza kutekelezwa, huku kipengele kingine kilichopitishwa na UEFA ni kubadili mfumo wa kuchezwa kwa fainali hizo kuanzia mwaka 2020.

Kuanzia mwaka huo UEFA itashuhudia fainali za mataifa ya barani Ulaya zikichezwa katika bara zima kwa kushirikisha miji iliyoshinda tenda ya kuwa wenyeji.

Bondia Manny Pacquiao kuzichapa na Amir Khan.

Bondia kutoka nchini England, Amir Khan huenda akapambana na Manny Pacquiao, baada ya kushindwa kutimiza ndoto zake za kupanda ulingoni na bingwa wa dunia Floyd Mayweather aliyetangaza kustaafu mwishoni mwa juma lililopita.

Mzungumzo kuhusu mpambano wa Khan dhidi ya Pacquiao yanaendelea kwa sasa kwa kushirikisha viongozi wa pande zote mbili.

Tayari tetesi zimeanza kujitokeza katika mitandao ya kijamii zikieleza kwamba huenda wawili hao wakakutana ulingoni mwezi Novemba mwaka huu huku wengine wakidai pambano hilo litakua la mwisho kwa Pacquiao ambaye tayari ameshaeleza itakapofika mwaka 2016 ataachana na mchezo wa masumbwi.

Khan amekua kimya tangu alipomkandamiza mpinzani wake kutoka nchini Marekani Chris Algieri mwezi may mwaka 2015, na alionyesha dhamira ya kutaka kupanda ulingoni dhidi ya Floyd Mayweather, lakini aliweka masharti ya kutaka kupewa nafasi ya kutimiza ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hata hivyo Khan, bado ameonyesha dhamira ya kumuhitaji Mayweather, kwa kusema anaamini atabadili msimamo wake wa kustaafu mchezo wa ndondi ili arejee ulingoni na kukamilisha pambano la 50 ambalo amependekeza limkutanishe nae.

Kwa upande wa Manny Pacquiao,
hajarejea tena ulingoni tangu alipopoteza kwa point dhidi ya Floyd Mayweather katika pambano lililounguruma May 02 mwaka huu.
Mayweather alitangaza kuachana na ndondi mara baada ya mpambano wake dhidi ya Andre Berto aliyemshinda kwa point.

Historia inaonyesha kwamba Mayweather anakua bondia aliyetangaza kujiweka pembeni huku akiwa ameshinda michezo 49 pasi na kupoteza hata mmoja.

Jennifer Hudson akolea kwa penzi la Mkenya.

Ni miaka sita sasa tangu wawili hawa wawe kwenye mahusiano huku wakijaliwa kupata mtoto wa kiume ambaye ana uri wa miaka mitano.

Pengine wengi walidhani muimbaji na muigizaji mwanadada Jennifer Hudson hatadumu kwenye penzi la mcheza miereka mwenye asili ya nchi ya Kenya David Otunga kutokana na mapenzi ya maisha ya kistaa kutokudumu lakini kwa upande wao mambo yanazidi kunyooka.

Inaripotiwa ili kuimarisha penzi lake, Jennifer Hudson hataki hata kumuachia na kuwa mbali na Baba mtoto wake huyo. Mapema jumatano wiki hii kamera za mapaparazi ziliwanasa wawili hao wakiwa pamoja kwenye mtoko tamasha la wiki ya mitindo na urembo huko marekani.

Obama amtetea Mtoto aliyeshikiliwa na Polisi kwa kutengeneza saa iliyodhaniwa bomu.

Mtoto Ahmed Mohamed (14) ameachiwa huru baada ya Rais Obama kumtetea kwa kuisifia na kutaka aipeleke Ikulu saa aliyobuni na kutengeneza na kusababisha ashikiliwe na polisi mjini Texas, ikidhaniwa ni bomu.
Unazungumziaje hili?

David Busst amtabiria Shaw kurudi mapema uwanjani.

Mchezaji Luke Shaw anateseka baada ya kuvunjika mfupa mara mbili katika mguu wake wa kulia Jumanne usiku.
Alikuwa akiitumikia timu yake katika michuano ya Champions League kwa timu yake ya Manchester United dhidi ya PSV.

Mchezaji wa zamani wa Coventry, David Busst anaamini Luke Shaw atarudi uwanjani kabla ya kuisha msimu huu
Busst aliwahi kuvunjika dimbani Old Trafford mwaka 1996, katika mchezo dhidi ya Coventry na United ambapo alimaliza soka lake miezi michache baadae.

Taarifa zinasema mchezaji huyo anaweza kurudi uwanjani baada ya miezi sita.

Toa mtazamo wako baada ya kuvunjika kwa Shaw mguu wake!

Chicharito ameanza kufunga Bayern Leverkusen.

Mchezaji wa zamani wa United, Javier Hernandez amefunga goli lake la kwanza kwa Bayer Leverkusen ya Ujerumani katika mchezo wa Champions League wa ushindi wa magoli
4 - 1 nyumbani dhidi ya ATE Borisov.

Huyu ndiye Mbuzi anayekunywa Chai ya Maziwa.

Mwandishi na mpiga picha Mohamed Jabra kutoka Gaalkayo, katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Somalia, eneo la Puntland, amesema baada ya mlo wa jioni jana, alikwenda kwenye mgahawa mmoja akiwa na rafiki yake na kuagiza vikombe viwili vya chai.

"Ghafla alitokea mbuzi na kutaka kunywa chai yangu," Mohamed alisema. "Nilijaribu kumzuia, lakini hakukubali, ikabidi nimuachie tu anywe chai yangu."

Amesema mbuzi huyo 'aligida' chai hiyo haraka haraka, licha ya kuwa ilikuwa ya moto.
"Ikabidi nijiliwaze kwamba, kwa kuwa chai yenyewe ilikuwa ya maziwa ya mbuzi, kwa hiyo alikuwa na haki ya kuing'ang'ania."