Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday, 6 June 2015

WARAKA KWA WANAVYUO VIKUU TANZANIA KUHUSU KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA NA KUSHIRIKI  KUPIGA KURA KWENYE UCHAGUZI MKUU OCTOBA 25/2015

Leo tarehe 5/6/2015, baadhi ya wanafunzi  kutoka vyuo vikuu tumeweza kuonana na m/kit wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Damian Lubuva.Ambayo ilikuwa ni makubaliano tuliyoyafanya juzi tarehe 3/06/2015 kuhusu kuonana nae.

Madhumuni ya kuonana na m/kiti wa NEC ,ni kama ifuatavyo

Moja ni kujua namna gani wanafunzi tunaweza kujiandikisha na kupata fursa ya kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.

Pili ni namna gani tutaweza kupiga kura ikiwa maeneo tuliyojiandikishia yatakuwa tofauti na ambapo tutakuwa wakati wa uchaguzi.

Mengine zaidi ya hayo tumeyaeleza kwenye WARAKA WETU KWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI(NEC).

Makubaliano yetu na Jaji Damiani Lubuva ni kama ifuatavyo

Moja wanafunzi wote wa vyuo vikuu atahakikisha tunajiandikisha na kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu maeno mbalimbali ambayo tutakuwa wakati wa uchaguzi......Pia swala hili limejieleza wazi katika ibara ya 5(3)(c) kwenye katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977

Pili WARAKA WETU KWA TUME YA UCHAGUZI(NEC), utajibiwa pia kwa maandishi tarehe 10/06/2015, baada ya kikao cha wajumbe wa Tume kukaa na kujadili namna gani wataweza kutuandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu.

Changamoto tulizokutana nazo ni

Viongozi wa shilikisho la vyuo vikuu Tanzania(TAHILISO) waliofika ofisi za tume ya uchaguzi(NEC), Kutaka kujaribu kukwamisha mazungumzo yetu na m/kiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva kwa malengo yao binafsi.

Lakini tunashukuru watendaji wa Tume ya uchaguzi(NEC) kwa pamoja na m/kiti wa NEC waliweza kuheshimu makubaliano yetu ya kufanya nao mazungumzo.

Hata hivyo viongozi hao wa TAHILISO walishindwa kujumuika nasi katika mazungumzo hayo na kutokomea kusikojulikana.

Wito wetu kwa Wanavyuo vikuu Tanzania tunahitaji ushirikiano kwa pamoja ili kuweza kufanikisha na sisi tunapata haki yetu ya msingi ya kikatiba kushiriki kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi wakitaifa tunao wataka na hatuwezi kuchagua viongozi hao kama tutakuwa hatujajiandikisha.

Wanafunzi walioshiri kwenye mazungumzo hayo ni wafuatao

1.)LUSEKELO  AMIMU-Chuo kikuu Ardhi
2.)BARAKA NYEUA-T.I.C.D Arusha
3.)NTILE  JOEL-UDSM
4.)PATRICK JOHN-UDSM
5.)MWIDADI  MSANGI-Ardhi
6.)FRANK JOASH-CPS &CPA
7.)SHIRIMA  JUVENAL-Ardhi
8.)SHITINDI  VENANCE-UDSM

Baada ya Tume ya uchaguzi NEC kutoa majibu kwa maandishi tutawaletea tena mrejesho kwenu.

Kwa mawasiliano zaidi:
0684-615128

Wakuta chura ndani ya kopo wa tomato

Mtu na mkewe waliokuwa wakiandaa chakula cha mchana walipigwa na butwaa walipopata chura kilichokuwa kimekufa ndani ya mkebe wa tomato.
Muhammad na Sanam Hussain waligundua hayo wakati bi Hussain alipokuwa akipika mchuzi katika nyumba yao huko Alum Rock mjini Birmigham.
Bi Hussain ambaye ni mjamzito wa miezi saba amesema kuwa anaugua baada ya kukiona kiumbe hicho ndani ya mkebe wa tomato.
Kampuni ya Euro Foods inayouza bidhaa hiyo imesema kuwa inachunguza ni vipi chura hicho kiliingia ndani ya mkebe huoBi Hussain amesema,''kwa kweli inachukiza ,nimeshtuka sana,nina wasiwasi kuhusu mtoto wangu kwa kuwa mimi ni mjamzito''.
''Nimeongea na mkunga wangu kuhusu niliyoyaona na akaniamibia niende hospitalini nitakaposikia vibaya.'',Mumewe amesema kuwa alishtushwa na makelele yaliopigwa na mkewe.
''Mke wangu alikuwa akiniandalia chakula cha mchana na mwanagun wa miezi 15 Wakati alipofungua mkebe huo alionekana na kuanza kupiga makelele akiniita''.

Henderson afurahia Brendan Rodgers kubaki Liverpool.

Kiungo Jordan Henderson amefurahia maamuzi ya uongozi kumbakisha kocha wa Liverpool Brendan Rodgers
Kapteni huyo amesisitiza watamaliza msimu ujao kwa mafanikio na kuiletea heshima timu hiyo.
Kocha Rodgers alikuwa na wakati mgumu baada ya matokeo yasiyofurahisha mwishoni mwa msimu na kushindwa kuwapa kikombe chochote.
Kwa kikosi cha sasa cha Liverpool kitaweza kushindana na miamba mingine ya soka katika mbio za ubingwa?

Falcao kutua Darajani

Mchezaji Radamel Falcao anayecheza kwa mkopo Old Trafford anataka kubaki kucheza Premier League. Mcolombia huyo ameshindwa kuishawishi Manchester United kumnunua jumla.
Falcao amefunga magoli manne tu Old Trafford, mchezaji huyo anataka kuchezea Chelsea msimu huu.Uwepo wa Eden Hazard, Diego Costa,Oscar, Willian, kutamshawishi Meneja Mourinho kumpa nafasi Falcao Stamford Bridge?

Raheem Sterling kuelekea Man United.

 
Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling huenda akaelekea katika kilabu ya Manchester United ,hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana wasiwasi kuhusu athari za uhamisho huo hususan kutokana na ushindani mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili.
Hatahivyo Liverpool imesema kuwa haiko tayari kufanya biashara na wapinzani wao wakuu kutoka Kaskazini Magharibi.
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Luois Van Gaal anavutiwa na kasi ya mchezaji huyo na uwezo wake wa kuwaponyoka mabeki.
Sterling amekataa ombi la kitita cha pauni laki moja kutoka kwa Liverpool akisema kuwa anataka kuondoka na kukichezea kilabu ambacho kina uwezo wa kushinda mataji.

Angel Di Maria "Nabaki old Trafford

Mchezaji raia wa Argentina Angel di Maria amethibitisha kubaki Manchester United msimu ujao.
Pamoja na tetesi za kujiunga PSG kwa ada ya ya Euro milioni 60.
Di Maria amefunga magoli manne na kutoa pasi za magoli 12 kwa mashindano yote.

Mesut Ozil ajinyakulia tuzo Ujerumani.

Mchezaji nyota wa Arsenal Mesut Ozil ameshinda tuzo ya balozi wa mpira wa Ujerumani 2015.
Mesut Ozil ametangazwa kuwa balozi wa mpira wa Ujerumani mapema wiki hii.Tuzo hii hutolewa kwa watu wanofanya kazi za kuitolea.Ozil, amesema tuzo hii ina mana kubwa kwake.

Rais wa Afrika Kusini ahusishwa kashfa ya rushwa FIFA.

Waziri wa michezo wa Afrika Kusini , Fikile Mbalula, sasa anasema rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki ndie aliyeruhusu ulipwaji wa fedha ,dola milioni 10 kwa FIFA , hela ambayo sasa inakumbwa na madai kwamba ilikuwa rushwa .
Utawala wa Afrika Kusini umekuwa ukisisitiza kwamba ulikuwa ni mchango wa kusaidia kukuza soka katika nchi za Caribbean.
Lakini waendesha mashtaka wa Marekani wanadai ilikuwa hongo, iliyoshawishi kupewa uenyeji wa kombe la dunia mwaka 2010 .
Bwana Mbeki mwenyewe hajatoa kauli yoyote kuhusiana na swala hilo.
Barua inayosemekana iliandikwa na shirikisho la soka nchini Afrika kusini , inaonekana kuongeza uzito kwenye shutuma kwamba serikali ya nchi hiyo ilitoa malipo hayo kwa siri.