Manchester
United imekubaliani Dili na Sporting Lisbon kumsaini Kiungo William
Carvalho ambae pia huchezea Timu ya Taifa ya Portugal.
Habari zilizovuja huko
England zinasema Mchezaji huyo Mzaliwa wa Luanda, Angola na ambae
alihamia Ureno akiwa bado mchanga, atahama kutoka Sporting Lisbon ya
Ureno kwenda Man United kwa Dau la Pauni Milioni 35 na tayari Uhamisho
ushatiwa Saini zote kwa Mkataba wa Miaka Mitano lakini utatangazwa rasmi
Dirisha la Uhamisho likifunguliwa.
William Carvalho, mwenye Miaka 22, ni
Kiungo mahiri ambae amekuwa akifukuziwa na Klabu za Real Madrid, Inter
Milan, Liverpool na Monaco lakini Man United wamewazidi kete kwa sababu wana
uhusiano mzuri na Wakala wake, Jorge Mendes, ambae pia ni Wakala wa
Cristiano Ronaldo.
Habari hizi pia zimedokeza Wachezaji
wawili wa Southampton, Adam Lallana na Luke Shaw, watafuata nyayo huku
Kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos, akiripotiwa kupewa Ofa ya Mshahara
wa Pauni 260,000 ikiwa atajiunga Man United.
Habari hizi za Toni Kroos zimeanza
kuaminika hasa baada ya Jana Bayern Munich kumsaini mbadala wa Kroos,
Kiungo kutoka Eintracht Frankfurt, Sebastian Rode, kwa Mkataba wa Miaka
minne.
Kroos, ambae Mkataba wake na Bayern unamalizika Mwakani, amegoma kusaini Mkataba mpya na Bayern.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari zote za michezo hususan tetesi za usajili barani ulaya na katika kipindi cha majira ya joto barani ulaya ambacho timu zinaenda kuimarisha vikosi vyao
0 comments:
Post a Comment