Barcelona
ina imani kubwa kuwa wataweza kusaini Wachezaji wapya mwishoni mwa
Msimu huu licha ya FIFA kuwafungia kutosaini Mchezaji yeyote mpya kwa
Vipindi viwili vya Usajili.
Barca walipewa Adhabu hiyo na FIFA baada
ya kukiuka Kanuni za kusaini Wachezaji 10 walio chini ya Umri wa Miaka
18 na Adhabu hiyo inadumu hadi Juni 2015.
Hata hivyo, Makamu wa Rais wa Barca,
Manel Arroyo, amewaambia Wanahabari kuwa Klabu yao inafanya kazi na
Shirikisho la Soka la Spain, RFEF, ili kukata Rufaa kupinga Adhabu ya
FIFA.
RFEF pia iliadhibiwa na FIFA kwa makosa hayo ya Barca kwa kupigwa Faini.
Arroyo amesema: “Tunaifanyia kazi Rufaa
ambayo itaturuhusu tufanye Usajili kwa kuiondoa Adhabu kwa muda. Tuna
hakika tutafanikiwa na mwishoni mwa Msimu tutapata Wachezaji wapya!”
Duru toka ndani ya Klabu ya Barcelona
zimedokeza kuwa ikiwa FIFA itaitupa Rufaa yao, wao wako tayari kupeleka
suala hili huko kwenye Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, CAS [Court of
Arbitration for Sport] ambako ipo desturi ya kuisimamisha Adhabu
inayolalamikiwa hadi wao watakapotoa Hukumu ya Rufaa,
Rufaa hizi zinaweza kuwapa fursa Barca
kukamilisha Dili ambazo sasa tayari zimefanikiwa kufikia makubaliano
zinazowahusu Kipa wa Borussia Moenchengladbach Marc-Andre ter Stergen na
Mchezaji wa Miaka 17 wa Croatia, Alen Halilovic, ambae anatimiza Miaka
18 Mwezi Juni.
0 comments:
Post a Comment