Facebook

Saturday 19 April 2014

Mr.Nice aweka wazi sababu zalizomfanya afulie .......soma hapa alichokisema.......


Mr_Nice_face_2
 

Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice, leo hii afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki, katika moja ya interview Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa kilichotokea ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu.Mr.nice alizidi kufunguka na kusema kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zote zikiwa katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo zimetoweka katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.

“kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali, naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu” alisema Mr.Nice.
 
“Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, South Africa na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana” Alimalizia star huyo kutoka Tz na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.



Lucas-Mkenda-aka-Mr-Nice
 


Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana enzi hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa yanamtoka kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda ambapo hadi waziri wa nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye red carpet huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki wake lukuki waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake.

0 comments:

Post a Comment