Facebook

Saturday 19 April 2014

Mabadiliko ya Uelekeo wa Barabara katikati ya Jiji la Dar Es Salaam Kuanzia 28/04/2014.....soma hapa...

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD

Key:
1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.

 2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way} 

 3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets} 

 4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala

 5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART

 6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko {Roundabout} 

 7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}



1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari
 (Askari Monument) hadi Clock Tower Magari  kutakuwa na
 mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock 
Tower badala ya Askari Monument. 




2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya 
Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa 
yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani 
tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station. 


3. Barabara ya Kivukoni  Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry
 itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).


4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean
 Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.


5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za  Makataba 
zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano 
ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya 
Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na 
kurudi Posta Mpya .


Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART

UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.

AU.

OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA

MABALA NA SHOPRITE SUPEEMARKET JIRANK NA KAMATA


Mtaarifu mwingine juu ya mabadiliko haya kuondoa usumbufu ifikapo siku ya Jumatatu 28/04/2014. PASAKA NJEMA

0 comments:

Post a Comment