Monday, 21 April 2014
Ndugu wanaoshirikiana kula nyama za watu wakamatwa............fuatilia hapa...................
Watu wawili wanaotuhumiwa kula nyama za binadamu wamekamatwa baada ya kichwa cha mtoto wa miaka mitatu, kukutwa katika nyumba wanayoishi nchini Pakistan.
Polisi waligundua tukio hilo la kutisha na kuwakamata watuhumiwa Mohammad Arif Ali (35) na mdogo wake Mohammad Farman Ali mwenye miaka 30.
Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Dailymail, wanandugu hao wanaotoka katika mji mdogo wa Darya Khan wamewahi kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kula nyama za binadamu. Waliachiwa huru baada ya kumaliza kutumikia adhabu hiyo mwaka jana.
Arif na Farman walikamatwa na kuswekwa rumande wakati uchunguzi ukiendelea, baada ya tukio hilo lililowavuta wengi na kutikisa tena eneo hilo.
Miaka mitatu iliyopita ndugu hao walifukua zaidi ya miili 100 ya maiti katika makaburi yaliyopo karibu na kijiji chao kisha kuzitumia maiti hizo kama asusa.
Mkuu wa Polisi katika eneo hilo, Ameer Abdullah alisema maofisa wake wa polisi waliamua kuvamia na kufanya upekuzi katika eneo hilo, baada ya majirani kulalamika kwamba kuna harufu mbaya ambayo imekuwa ikitoka katika nyumba waliyokuwa wakiishi.
“Wakazi hao waliifahamisha polisi baada ya kusikia harufu mbaya ikitokea katika nyumba waliyokuwa wakiishi watu hawa,” alisema Abdullah.
Abdullah alisema: “Tulifika katika nyumba hiyo siku ya Jumatatu asubuhi na kufanya upekuzi kabla ya kukiona kichwa cha mtoto wa miaka mitatu.
“Baada ya kugundua kitu hicho kinachotisha, tulimkamata mmoja wa ndugu hawa Mohammad Arif na alitupatia ushirikiano hadi tulipomweka kizuizini ndugu yake,” alisema Abdullah.
Alisema jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi ili kung’amua iwapo kuna makaburi mengine yamechimbwa na watu hao kijijini hapo au katika vijiji vya jirani.
Baada ya kuulizwa maswali mengi na polisi, ndugu hao walikiri kula nyama za watu na kueleza ukweli namna walivyokuwa wakitengeneza mlo huo. Kwa kuwa Pakistan haina sheria zinazohusu ukatili wa maiti, huenda haitakuwa rahisi kwa wawili hao kufungwa jela maisha.
Related Posts:
AL Shabab watangaza sheria ya mavazi ! Kundi la al-Shabab limewakamata wanawake takriban 100 na kuwataka kuvaa nguo kwa mujibu wa dini ya Kiislam, vinginevyo watapigwa mikwaju. Wanawake hao walikamatwa katika mji wa Buale, karibu kilomita 300 kusini… Read More
Rais wa zamani wa Ivory Coast,Gbagbo kushtakiwa na ICC Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imetangaza mipango ya kutaka kumshtaki rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo. Gbagbo anatuhumiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi alioshindwa mwaka 20… Read More
Uingereza yaahidi kusaidia Nigeria Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekahu. Kundi lake linawazuia wasichana zaidi ya miambili Uingereza imetangaza kuwa itaongeza msaada wake wa kijeshi na kielimu kwa Nigeria ili kuisadia katika juhudi za kupambana n… Read More
Msichana mwingine ajinyonga India Wanawake wa India wapinga ubakaji ambao umekithiri mno India Msichana mmoja mwenye umri mdogo amepatikana akining'inia mtini Kaskazini mwa India. Familia … Read More
Mwanakikundi wa Mafia "Mafioso" ataka kuungama kwa Papa. Kigogo mmoja wa zamani wa kundi la mafia amemuandikia barua Baba Mtakatifu, akiomba kwenda kuungama na kukiri "siri tatu muhimu sana" ikiwemo moja maarufu nchini Italia ya kupotea kwa mtoto. Katika barua hiyo yenye … Read More
0 comments:
Post a Comment