Facebook

Saturday, 19 April 2014

Rais wa FIFA,Sepp Blatter ai[pongeza Azam kutwaa ubingwa Tanzania....soma hapa.....


Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Sepp Blatter ametuma salamu za pongezi kwa mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Azam FC.

Blatter ameandika barua hiyo kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na kutoa pongezi hizo.
Amewapongeza benchi la ufundi pamoja na wachezaji kutokana na kuweka rekodi mpya ya bingwa tofauti.
Malinzi amethibitisha kupokea barua hiyo ya Blatter na kusema atawakabidhi Azam FC, kesho.
Aidha, Malinzi naye ametuma pongezi hizo za ubingwa kwa Azam FC.

“Tutawakabidhi barua huyo ya Blatter kutoka Fifa, lakini tunawapongeza kutokana na kutwaa ubingwa,” alisema Malinzi.

0 comments:

Post a Comment