Facebook

Friday, 18 April 2014

Rapper Maarufu ajikata kiungo cha siri makusudi,Madaktari washindwa kuunganisha.......fuatilia hapa......


Rapper mwenye uhusiano na kundi la Wu-Tang Clan, Andre Johnson hana tena kiungo kinachomfanya aitwe mwanaume kwakuwa madaktari wameshindwa kuunganisha.

  Johnson aka Christ Bearer aliukata uume wake jana Jumatano na kujirusha kwenye nyumba ya ghorofa mbili anakoishi huko North Hollywood kwa kile kinachodaiwa kutaka kujiua. Alikimbizwa kwenye hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center lakini uume wake umedaiwa kukatika kabisa.

Johnson/Christ Bearer ni miongoni mwa rapper wa kundi liitwalo Northstar, lilioanzishwa na rapper Wu-Tang Clan, RZA. Kulikuwepo na rappers wengine kwenye tukio hilo waliokanusha kuwepo na madawa ya kulevya kiasi cha kumfanya achukue uamuzi huo. Wanaamini kuwa Johnson/Christ Bearer anaweza kuwa na matatizo ya kiakili.

0 comments:

Post a Comment