Facebook

Friday, 18 April 2014

Jay Dee Alalamikiwa na Jirani zake.....fuatilia hapa kujua kisa ni nini???.......



MAJIRANI wanaoishi karibu na mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Judith Wambura ‘Jide’ Gladness Mallya na Hamida Hassan wamelalamika kwamba mwanamuziki huyo ameiweka nyumba yake katika mazingira ya uchafu yanayohatarisha maisha yao.

Jay Dee anaeishi na Majirani hao wanaoishi Kimara-Temboni jijini Dar, Majirani hao walisema mwanadada huyo ameacha vichaka vikubwa vinavyoizunguka nyumba yake hali ambayo ni hatari kwani nyoka wanaweza kufanya makazi hivyo kusababisha maafa kwa watoto na watu wazima.

“Yaani huyu mwanamuziki Jaydee ametuachia kichaka, yeye na mumewe hawataki kufanya usafi kuizunguka nyumba yao hali ambayo inatupa wasiwasi sisi majirani, tuna watoto wanaweza kung’atwa na nyoka kwani nyoka hupenda kuzaliana kwenye vichaka kama hivi,”


Waliendelea kusema kuwa, Jide hana mfanyakazi wa ndani wala ndugu yeyote anayeishi naye, inawezekana ndiyo maana anashindwa kufanya usafi kuzunguka nyumba yake.

“Lady Jaydee anaishi na mumewe (Gardner) tu labda ndiyo sababu ya kushindwa kutunza mazingira, majani yameota mpaka kero. Tumeshapeleka malalamiko yetu serikali ya mtaa lakini hajaitwa kuambiwa, tunashangaa,” alisema jirani huyo.




 Baadae Mumewe alihojiwa ..............
  Gardner alijibu:
“Kama wamesema hivyo mimi sina la kujibu (no comment)”.
  Na inasemekana walifika kwenye ofisi ya serikali ya mtaa lakini ilikuwa imefungwa.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kufahamu maovu mbalimbali yaliyojificha yanayofanywa na wasanii 

0 comments:

Post a Comment