Facebook

Thursday, 17 April 2014

Baada ya watoto kutekwa na Boko Haram wazazi wao waingia msituni Kuwasaka Nigeria

 
Wazazi wa takriban watoto miamoja waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram wameingia msituni kuwatafuta watoto wao.
Wasichana hao walitekwa nyara kutoka shuleni mwao katika eneo moja la vijijini Kaskazini Mashariki mwa Nigeria Jumatatu usiku.
Inasemekana kuwa ni hatari sana kwa wazazi hao hata kutafakari kuingia msituni , kwani wapiganaji wa Boko Haram wamewaua mamia ya watu mwaka huu , kwa kuwakata vichwa vyao.
Rais Goodluck Jonathan, anakutana na magavana wa majimbo na maafisa wakuu wa jeshi kujadili swala la usalama.
Awali jeshi lilisema ni wasichana 18 pekee kati ya 129 waliotekwa nyara bado hawajapatikana .
Wengine wote walifanikiwa kutoroka kutoka mikononi mwa Boko Haram.
Lakini wazazi wanapinga kauli ya jeshi na wanasema kuwa wasichana wengi bado hawajulikani waliko.
Wapiganaji hao waliwateka nyara wasichana kutoka shule ya wabweni walipokuwa wanajiandaa kwa mitihani yao.

Taarifa zinasema ni wasichana 17 pekee waliofanikiwa kutoroka kinyume na kauli ya jeshi.
Inaanimika kuwa wapiganaji wa Boko Haram ndio wamewateka nyara wasichana hao na kuwapeleka katika msitu ulio karibu na mpaka wa Nigeria na Cameroon.
Kundi hilo linapiga vita serikali ya Nigeria likisema kuwa linataka nchi hiyo itawaliwe kwa misingi ya kiisilamu.
Jumatano watu 18 waliuawa katika shambulizi lililofanywa wilayani Gwoza Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wadadisi wanasema shambulizi dhidi ya wasichana ni jambo la aibu kubwa kwa serikali
Taarifa ya jeshi ilisema kuwa wasichana wengi walifanikiwa kutoroka ingawa wazazi wanakana madai hayo wakisisitiza kuwa wasichana wengi bado hawajapatikana

Related Posts:

  • Bomu laua watu 6 katika makao ya Rais Somalia.Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka karibu na lango kuu la jumba la rais katika mji mkuu wa Mogadishu. Takriban watu sita wamefariki,ikiwemo walinzi wa rais.Raia mmoja wa Uturuki pia aliuawa. Wengine 10 waliripotiwa kuj… Read More
  • Panya wasababisha kifo 'Jela ya Mandela'Watu karibu 4,000 wameondolewa kutoka jela ya Pollsmoor nchini Afrika Kusini baada ya panya wengi kuvamia gereza hilo na kusababisha kifo cha mfungwa mmoja. Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela aliwahi kufungwa kati… Read More
  • " Game of Thrones" yajinyakulia tuzo kubwa Marekani. Tamasha kubwa la kila mwaka Emmys Awards, la kutoa tuzo kwa vipindi vya televisheni limefanyika mjini Los Angeles Marekani. Kipindi cha Game of Thrones, kimenyakua matuzo mengi zaidi ikiwemo makala bora zaidi. Viola Davis nay… Read More
  • Papa awasili Marekani apokewa na ObamaKiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani katika siku ya kwanza ya ziara ya kihistoria nchini humo ambapo amelakiwa na Rais wa nchi hiyo Barack Obama. Papa Francis aliwasili kwenye uwanja wa n… Read More
  • Wanasayansi watengeneza figo maabara. Je una matatizo ya figo ? Ikiwa jibu lako ni ndiyo kuwa na subira, maanake hivi karibuni figo zilizoundwa kwenye viwanda na maabara vitakuwepo kuwasaidia. Nafahamu kuwa waganga wengi wamewaahidi tiba lakini hii sio hekaya tu… Read More

0 comments:

Post a Comment