Maombi ya kocha ,wa Arsenal Arsene Wenger ya kuitaka
Everton ipoteze mchezo ili kuisaidia timu yake kufuzu kuweza kushiriki kombe la ligi ya mabingwa
msimu ujao yalitimia hapo jana ,Crystal Palace ilipoilaza Everton mabao
3-2 na
kuiruhusu Arsenal kusalia katika nafasi ya nne ikiwa na alama 67 alama moja zaidi ya Everton.Man City 2-2 Sunderland
Katika mechi nyingine iliyochezwa jana usiku ,uwezekano Manchester City kutwaa kombe la ligi hiyo ya Uingereza uliyeyuka pigo baada ya timu hiyo kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Sunderland.
Bao la kwanza lilipachikwa wavuni na Fernandinho kunako dakika ya 2.
Sunderland ilisawazisha kunako dakika ya 73 na kuongeza lingine dakika kumi baadaye kupitia kwa mchezaji Wikham.
Kutokana na matokeo hayo Pelligrini sasa anategemea matokeo ya vinara wa ligi hiyo Liverpool na Chelsea kubaini matumani yake ya kutwaa taji la mwaka huu.
The Reds ndio wanaoongoza jedwali la ligi na alama 77 ikifuatiwa na Chelsea ikiwa na alama 75.
Man city inashikilia nambari ya tatu kwa alama 71.
Ratiba ya Man City
- Mon 21 April: v West Brom (H)
- Sun 27 April: v Crystal Palace (A)
- Sat 3 May: v Everton (A)
- Wed 7 May: v Aston Villa (H)
- Sun 11 May: v West Ham (H)
0 comments:
Post a Comment