Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Wednesday, 8 April 2015

IFAHAMU HISTORIA YA KLABU YA ARSENAL FC.

Mwanzo hadi Vita ya Kwanza ya Dunia
Maisha ya klabu ya soka ya Arsenal yalianza pale
kikundi cha wafanyakazi katika kiwanda cha
kuzalisha zana za kivita cha Woolwich
walipoamua kuunda klabu ya soka mwishoni
mwa mwaka 1886. Klabu ikawa ikishiriki michezo
huku ikijulikana kama Dial Square. Mchezo wao
wa kwanza waliifunga timu ya Eastern Wanderers
6-0, tarehe 11 Desemba 1886.

Baada ya muda mfupi, jina likabadilishwa na kuwa
Royal Arsenal huku timu ikiendelea kushiriki katika
michezo ya kirafiki na mashindano ya nyumbani kwa
kipindi cha miaka michache iliyofuata.

Mwaka 1891 klabu ikawa ya kulipwa na kubadilisha
jina na kuitwa Woolwich Arsenal na hatimaye
kujiunga na ligi ya soka mwaka 1893. ‘Washika
bunduki’ hao wakahamia Highbury mwaka 1913 kama
timu ya ligi daraja la pili. Baada ya Vita ya Kwanza ya
Dunia, Arsenal wakapigiwa kura na kuingizwa katika
ligi daraja la kwanza, iliyokuwa imeongezwa ukubwa,
ambako wameendelea kudumu hadi leo.
Chapman na kipindi cha mafanikio miaka ya 1930

Itaendelea

Imeandaliwa na Emmanuel Noel.

COPA ITALIA : JUVE WAINYUKA FIORENTINA 3-0, HAO FAINALI !!

Wakicheza Ugenini bila ya Nyota wao bora,
Andrea Pirlo , Paul Pogba na Carlos Tevez,
Juventus , chini ya Kocha Massimiliano
Allegri, Usiku huu wameipindua kipigo cha
mechi ya kwanza na kuichapa Fiorentina
3-0 na kutinga Fainali ya Coppa Italiana.

Hii ni nafasi murua kwa Juve kutwaa Dabo
Msimu huu kwani kwenye Ligi Serie A wao
ndio Vinara wakiwa Pointi 14 mbele .

Bao za Juve, ambao walifungwa 2- 1 katika
Mechi ya kwanza zilifungwa na Alessandro
Matri , Roberto Pereyra na Leonardo
Bonucci.

Tuesday, 7 April 2015

FALCAO NA MAWAZO YAKE MENGII.

Ni shabiki gani wa Manchetser United atasimama na kusema Man United isimpe mkataba Falcao endapo atatupia magoli dhidi ya Man City, Chelsea na Arsenal??

Hivi unajua ni kiasi gani Falcao anapenda kuendelea kuishi mjini Manchester? Kichwa chake chenye nywele nyingi kinajua kifanyeje ili mwisho wa msimu akae meza moja na Ed Woodward pembeni yake wakala wake Jorge Mendes wakijadili kuhusu mkataba wake mpya.

Bahati mbaya hawezi pata namba kikosi cha kwanza lakini miguu yake itaongozwa na kichwa chake kufanya kinachotakiwa kwa dakika atakazopewa.

Van Persie hayupo lakini bado hajapata bahati ya kuaminiwa, anajua fika akifunga tu game ijayo ataanza na Man United wataimba sana jina lake

Anakumbuka alivyoipa Man United goli la ushindi dhidi ya Everton na jinsi alivyotukuzwa, kuwafunga Aston Villa sio dili ila akiwapiga City ufalme utakuwa wake kama Mata alivyojipa ufalme kwa kuwapiga Liverpool

Hivi umeahawahi jiuliza kitu gani kipo Man United sasa? Kwa taarifa yako kuna wachezaji watatu tu ambao wana uhakika kuwa kikosi cha kwanza.

De Gea,Carrick na Rooney hawa kina Mata,Fellain,Young,Valencia wamekuwa katika kikosi kufuatia juhud zao za hivi karibuni na wanapambana kila game sababu wanajua wakichemka kuna watu wanachoma mahindi pembeni

Achana na Blind,Herrera na Rojo ambao sasa ndo wana dhihirisha thamani zao,  Nakumbuka wakati Di maria anapata namba kikosi cha kwanza Young alikuwa injury alipopona alisema

"Narejea kuchukua namba yangu" mashabiki wa Man United na vyombo vya habari walimcheka na kumuona chizi walisahau hata Rooney aliwahi wekwa benchi na Welbeck dhidi ya Madrid

Huu ni wakati ambao wachezaji wa Man United wapo katika presha kubwa kila anaepata nafasi anataka kuonesha alistahili, na ili uoneshe wewe ni bora game za kuonyesha ni kama dhidi ya City.

Hata bongo mchezaji akifunga katika mechi ya watani anapata heshima na jina kubwa.

Di maria atataka kuonesha ni bora kuliko Young.
Namtazama sana Falcao sijui kwanini naona kama hii mechi itampa mkataba mpya ngoja tusubiri na tuone
……………………………………………………………………………
Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa makala nzuri na za kuvutia.

Imeandaliwa na EMMANUEL NOEL

Sunday, 5 April 2015

KARIBU KATIKA MKATE WA PASAKA,NIKIBURUDIKA NA LIGI KUU UINGEREZA.

Jana baada ya kuona Majina ya wachezaji katika mechi ya Arsenal na Liverpool niliona vitu viwili kwa haraka haraka, kwanza ni makocha kuwapanga watu wawili wenye bahati nzuri na timu zao msimu huu!!,

Kwa Arsenal alikuwepo Ozil na kwa liverpool alikuwepo Lucas Leiva.Ozil tangu arudi kutoka Majeruhi kwenye mechi alizocheza Arsenal wamechukua Alama 27 kati 30 ukijumlisha na Alama za mechi ya Jana kwa Upande wa Lucas , kwenye mechi zote alizoanzishwa za ligi mwaka liverpool haijawahi kupoteza.

kwa kuangalia hivyo utaona ni njinsi gani wachezaji hawa wanabahati ya matokeo mazuri na timu zao!!, nilisubiri kuona nani ana nyota kali!!, kwenye mechi ya kwanza kati liverpool na Arsenal , lucas ni mmoja wa viungo waliocheza vizuri sana siku ile, Dakika 15 za mechi ya jana Lucas alikuwa anapoteza mipira mingi kwenye eneo la timu yake , hii ilisababishwa na vitu viwili vikubwa , cha kwanza Viungo wa Arsenal katika dakika 15 za mwanzo walikuwa kwenye kiwango cha juu na hii ilitokana na lengo lao la kupata goli la mapema na hii ilitia hofu kwa viungo wa liverpool hasa hasa Lucas aliyepoteza mipira mitatu ya wazi  kwenye robo yake.

kitu kingine kilichosababisha Lucas asiwepo kwenye kiwango chake kulinganisha na mechi ya Liverpool na Arsenal pale Anfield ni kuwepo nje ya uwanja kwa muda mrefu , ilikuwa karata iliyoshabihiana na karata  aliyocheza Big Sam kwa Wiston Reid aliyekuwa nje kwa majeraha na mwisho wa siku karata yake kutofanikiwa na Reid kupata kadi ya njano.

Kitu kingine nilichokiona baada ya kuona orodha ya wachezaji ni baada ya kumuona Toure. Nilisubiri kuona kama Toure ataweza kupangua maneno yangu niliyosema siku baada ya Martin kupewa adhabu na FA ya Uingereza kuwa kuna madhara makubwa kama Toure Akipangwa kama beki wa kati kama mtu wa kuziba pengo la Martin, nilisema kwa kuziba hili pengo lazima liverpool wangebadili mfumo kutoka ule wa kuchezesha mabeki watatu mpaka mabeki wanne, Martin ndo mhimili wa mfumo wa mabeki wa tatu pale Liverpool, kweli nilichotegemea ndo kilichotokea, Toure hakuwa kiongozi kwa Can na Sakho hasa hasa kipindi cha kwanza, pia hakuendana na kasi ya mchezo , angalia goli la Sanchez , Giroud kitu utakachogundua Toure hakuwa mtu sahihi kuziba pengo la Martin, kipindi cha pili  Brendan Rodgers aliamua kuchezesha mabeki wanne , Sakho akawa na Toure hii ilisaidia kiasi fulani kupunguza makosa binafsi ya Toure , ila kama Toure angeendelea kucheza kama beki pekee wa kati basi Arsenal walikuwa na uwezo wa kuzirudisha goli 8 walizowahi kupingwa na Manchester united.

Tukiizungumzia Manchester United, Kwa mtazamo wangu unaweza ukaifananisha na duka linaloshindana na maduka mengine.
Carrick ndo Afisa mipango wa hilo duka yeye ndo anakuja na mipango jinsi gani duka liendeshwe , Herrera yeye ni wale kwenye Filamu tunawaita " STORY DEVELOPER "

Baada ya kupokea mipango ya bwana Carrick yeye ndiyo anaiendeleza na kuikuza ile mipango yeye ndiyo anayeamua Bidhaa yani "Mipira" iende wapi kwa Mata,Young na Rooney.

Fellaini ni jambazi mvuruga mipango,lililoajiriwa kwenye duka la bwana Van Gaal, Jambazi hili hufanya kazi moja, ya kwenda kwenye maduka jirani ambayo ni washindani wake na kuwabadilishia bidhaa zilizo na soko kwa bidhaa zisizo na soko kwa mfano, Kuchukuwa Whitedent na kuwawekea AHA.

Ukiangalia upande wa kushoto kwa Manchester United, utamuona Evra mweupe, Ila wanatofauti ndogo sana na Evra mweusi huyu mweupe anakaba vizuri kwa akili afu anashambulia kwa tahadhari na kwa akili nyingi, Evra mweusi alikuwa anakaba na kushambulia kwa kasi kubwa kuzidi huyu Evra mweupe ambaye ameleta uhai eneo la kushoto la Manchester united kwa siku za hivi karibuni.

Tofauti na Chenga zake, Kuminya mabeki lakini Young hana madhara makubwa ukilinganisha na Di Maria, Kuna kipindi Di maria akiwa uwanjani unaiona Manchester united hatari, Young krosi zake nyingi hazimfikii mshambuliaji,

Di Maria krosi zake nyingi zinazmfikia mshambuliaji.
Kuna Faida kubwa kuwaanzisha wote Mata na Di Maria kuliko kuwaanzisha Mata na Young.

Chelsea wamekuwa watumwa wa ligi huwezi kuwatofautisha na QPR, BURNELY, LEICESTER CITY, wamekuwa wakitumia nguvu nyingi ili kupata matokeo, nguvu walizotumia kwenye   nusu ya msimu huu zimeongezeka  sana na huku wachezaji wao wengi waliotumika sana msimu huu kuonekana kuchoka, kama ulibahatika kuangalia mechi dhidi ya Burnely waliyotoka sare, mechi dhidi ya Hull City waliyoshinda 3-2 na hii ya Jana dhidi ya Stoke wamekuwa wakitumia nguvu nyingi sana hasa hasa wakitizama nyuma moto wa Manchester city na United, na Arsenal.

Kuna kitu kimoja unatakiwa ukifahamu , mambo anayoyafanya Hazard yameshafanywa kipindi cha nyuma na J.COLE kipindi cha Claudio Ranieri wanachotofautiana ni kitu kidogo , wimbo wa Hazard unaimbwa sana midomoni mwa watu!!, ilihali wimbo wa J.Cole haikuimbwa sana midomoni mwa watu.

Kati ya mtu ambaye atakula pasaka na tumaini jipya la kutokushuka daraja wa kwanza kabisaa ni kocha wa Leicester city Nigel Pearson wa pili basi ni yule wa QPR.

Pasaka njema wapendwa ngoja mimi nibaki naburudika kuangalia marudio ya magoli ya Giroud, Sanchez, Ozil, Adam , Esteban Cambiasso, Zamora , Gomis , Rooney,Herrera,Vargas.Ndo magoli bora kwangu yaliyofungwa jana,nkimaliza magoli nitamalizia na saves za Tim Howard

Ahsanteni Mungu Awabariki.

#Martin kiyumbi.
0657771077

Saturday, 4 April 2015

Uchambuzi Mechi zote kali Ligi Kuu Uingereza leo Jumamosi.

Baada ya mapumziko ya siku kadhaa kupisha mechi za kirafiki za timu za Taifa pamoja na michezo ya kugombea kucheza kombe la mataifa Ulaya litakalo fanyika Ufaransa mwakani ligi mbalimbali zina endelea wikiendi hii.
  
      ARSENAL vs LIVERPOOL
                  14:45
     MAN UTD vs A.VILLA
                  17:00
      CHELSEA vs STOKE
                  19:30

    Tukianzia ktk dimba la Emirates Arsenal walio nafasi ya 3 kwa pointi 60 watacheza dhidi ya Liver walio nafasi ya 5 kwa pointi 54.
     Kuelekea ktk mchezo huo Arsenal wameshinda michezo 5 huku Liver wakishida michezo 4 na kupoteza 1 mbele ya Utd kwa mara ya kwanza tangu mwaka huu uanze.
      Arsenal wapo ktk kiwango bora hivi sasa wakiongozwa na Giroud mchezaji bora wa mwezi uliopita pamoja na Wenger akiwa kocha bora wa mwezi mara ya mwisho kupoteza ktk ligi ilikuwa mbele ya Spurs (2-1) mwezi wa pili tangu hapo wamekuwa na matokeo mazuri michezo 10 wamepoteza mara 1.
     Liverpool sio wabaya kwani kabla ya kupoteza dhidi ya Man Utd walikuwa hawajapoteza, kiwango dhohofu kilipelekea kupoteza mchezo huo wataingia kwenye mchezo huu kwa presha ya kuendelea kusaka nafasi 4 za juu huku bado wakiendelea tafakari kauli tata ya Sterling.
    Mchezo uliopita kati ya timu hizi tulishuhudia sare ya (2-2) lakini kwa upande mwingine hawajawa na matokeo mazuri  pale Emirates kwani wameshinda mara 1 kati ya 18 ktk michuano mbalimbali ( W1,D7,L10) pia ni mchezo mmoja tu ambao hawajaruhusu goli mbele ya Arsenal pale Emirates hivyo kutokana na takwimu hizi na hali ya msimamo ilivyo mchezo utakuwa mgumu sana upande wao.
    Huu ndo mchezo wenye hatrick nyingi ktk ligi (5)  asilimia kubwa Arsenal wana nafasi ya kushinda kulingana na kuimalika kila siku huku chagizo likiwa ni kupata pointi 3 na kukwea hadi nafasi ya 2 ya msimamo wa ligi (63 pointi, City 61).

    Licha ya Arteta,Debuchy,Diaby na Wilshere kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Brentford bado watakuwa na nafasi ndogo kuanza dhidi ya Liver hivyo tutaraji kikosi kilekile kilicho cheza michezo ya hivi karibuni ingawa kwa Welbeck haija julikana kutokana na maumivu aliyo yapata kwenye mchezo dhidi ya Lithuania ktk timu yake ya taifa, upande wa Liver watamkosa Skirtel na Gerrard.

---------

    Ni wachache sana walio ipa Utd nafasi ya kufika hapa walipo pointi 59 nafasi ya 4 na wakishinda mchezo huu watakwea hadi nafasi ya 2 kwa pointi 62 na itakuwa kwa mara ya kwanza ktk kipindi kirefu.
   Ushindi mbele ya Liver ambayo ilikuwa na matokeo mazuri mwaka huu inaweza kuwa ni chachu ya kikosi cha Van Gaal kufanya vyema mbele Villa iliyo nafasi ya 16-28 chini ya Tim Sherwood.
   Tutaraji kukiona kikosi kilekile kilicho cheza dhidi ya Liver huku kikichagizwa na kiwango bora cha Mata na safu ya kiungo.
    Villa watamkosa Cleverley kwani ni mchezaji alie kwa mkopo toka Utd, zaidi ya hapo kikosi chote kilicho cheza mechi za hivi karibuni kipo fiti.
     Hawana matokeo mazuri mbele ya Man Utd mchezo wa awamu ya kwanza ulio kuwa na kasi sana pale Villa Park ilikuwa sare ya 1-1 ( Benteke,Falcao) kwenye michezo 11 wameshindwa kupata pointi tatu huku ushindi wao wa mwisho ukiwa ni 2009 kwa goli la Agbonlahor.
   Villa wata ingia kwa mashambulizi ya kustukiza huku macho yao yakiwa kwa ( Sinclair,Benteke,Agbonlahor) ambao watakuwa mwiba mbele ya safu ya Utd.
   Licha ya kutokuonyesha kiwango mchezo dhidi ya Liver Rooney amekuwa na takwimu nzuri mbele ya Villa amefunga mara nyingi (12).

-------

   Wakiwa nafasi ya 10 kwa pointi 42 huku akichagizwa na matumaini ya mkataba mpya (3yrs) Mark Hughes atakuwa London kucheza dhidi ya wenyeji wake Chelsea walio kileleni kwa pointi 67 na mchezo 1 wa kiporo.
    Stoke watamkosa Moses kwani ni mchezaji wa Chelsea alie kwa mkopo hivyo tegemezi litakuwa hasa kwa Crouch anaetafuta rekodi ya wingi wa mabao ya kichwa kumfikia ( Alan Shearer-46) .
   Chelsea wameshinda mara 10 kati ya 13 dhidi ya Stoke wakipoteza mchezo 1,hawajaruhusu goli michezo 6 kati ya 7 dhidi ya Stoke.

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

Friday, 3 April 2015

Mtangazaji nguli wa BBC SWAHILI,Charles Hillary ajiunga na kituo cha AzamTv

Katika kile kinachoitwa mageuzi ya tasnia ya habari nchini.Kituo bora cha AzamTv kimefanikiwa kumnasa mtangazaji nguli wa Kituo cha BBC SWAHILI,Charles Hillary.

Tunasubiri makubwa kutoka AzamTv kutokana na utawala bora walionao hasa kuruhusu Weledi kufanya kazi.

Wednesday, 1 April 2015

SIMBA SC YAINGIA MIKATABA NA MAKAMPUNI MAKUBWA.

Huu Mkataba wa Simba na EAG kama umeanza kueleweka vile ila tatizo tunapata kigugumizi katika utendaji wa viongozi wetu lakini wakitulia na kufanya kile kinachostahiki watanufaika sana na hii kampuni.

Wemesaini mkataba na Huawei pamoja na MO Cola, wanataka kutuaminisha kama walikuwa wanajipanga.

Msimu ujao watakuja kivingine kwa sababu kwa waliofuatilia interview ya Mh.Kaburu alidai hawakuwa na mipango ya Ubingwa msimu huu bali wanaiandaa timu zaidi kwa msimu ujao ngoja nisubiri kama itakuwa kweli au ndo zile siasa za Tz.

BantuTz MAGAZETINI:SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA KURASA ZA MAGAZETI YOTE YA LEO APRIL 1,2014.

. 

BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa katika kurasa za mbele na nyuma magazeti yote ya leo.
 
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Endelea kufurahia huduma za BantuTz.com huku ukiusubiria kwa hamu Mtandao wa kijamii mkubwa na wa kisasa zaidi uitwao Bantuz mwaka huu