Facebook

Tuesday 7 April 2015

FALCAO NA MAWAZO YAKE MENGII.

Ni shabiki gani wa Manchetser United atasimama na kusema Man United isimpe mkataba Falcao endapo atatupia magoli dhidi ya Man City, Chelsea na Arsenal??

Hivi unajua ni kiasi gani Falcao anapenda kuendelea kuishi mjini Manchester? Kichwa chake chenye nywele nyingi kinajua kifanyeje ili mwisho wa msimu akae meza moja na Ed Woodward pembeni yake wakala wake Jorge Mendes wakijadili kuhusu mkataba wake mpya.

Bahati mbaya hawezi pata namba kikosi cha kwanza lakini miguu yake itaongozwa na kichwa chake kufanya kinachotakiwa kwa dakika atakazopewa.

Van Persie hayupo lakini bado hajapata bahati ya kuaminiwa, anajua fika akifunga tu game ijayo ataanza na Man United wataimba sana jina lake

Anakumbuka alivyoipa Man United goli la ushindi dhidi ya Everton na jinsi alivyotukuzwa, kuwafunga Aston Villa sio dili ila akiwapiga City ufalme utakuwa wake kama Mata alivyojipa ufalme kwa kuwapiga Liverpool

Hivi umeahawahi jiuliza kitu gani kipo Man United sasa? Kwa taarifa yako kuna wachezaji watatu tu ambao wana uhakika kuwa kikosi cha kwanza.

De Gea,Carrick na Rooney hawa kina Mata,Fellain,Young,Valencia wamekuwa katika kikosi kufuatia juhud zao za hivi karibuni na wanapambana kila game sababu wanajua wakichemka kuna watu wanachoma mahindi pembeni

Achana na Blind,Herrera na Rojo ambao sasa ndo wana dhihirisha thamani zao,  Nakumbuka wakati Di maria anapata namba kikosi cha kwanza Young alikuwa injury alipopona alisema

"Narejea kuchukua namba yangu" mashabiki wa Man United na vyombo vya habari walimcheka na kumuona chizi walisahau hata Rooney aliwahi wekwa benchi na Welbeck dhidi ya Madrid

Huu ni wakati ambao wachezaji wa Man United wapo katika presha kubwa kila anaepata nafasi anataka kuonesha alistahili, na ili uoneshe wewe ni bora game za kuonyesha ni kama dhidi ya City.

Hata bongo mchezaji akifunga katika mechi ya watani anapata heshima na jina kubwa.

Di maria atataka kuonesha ni bora kuliko Young.
Namtazama sana Falcao sijui kwanini naona kama hii mechi itampa mkataba mpya ngoja tusubiri na tuone
……………………………………………………………………………
Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa makala nzuri na za kuvutia.

Imeandaliwa na EMMANUEL NOEL

0 comments:

Post a Comment