Facebook

Saturday 30 May 2015

Tathmini ya Timu ya Arsenal msimu wa 2014-2015

Timu Arsenal imeonesha kuimarika msimu huu lakini imeshindwa tena kubeba kombe la ligi kuu ya Uingereza na kubaki na changamoto zilezile za siku zote.
Arsenal imemaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi 75 kwa michezo 38 huku ikishinda michezo 22 na kutoka sare mechi 9 na kufungwa michezo 7 pekee pamoja na kujikusanyia magoli ya kufunga 71 na ya kufungwa 36.
Timu hiyo ya Arsenal inatarajia kucheza mchezo wa fainali ya kombe la FA na Aston Villa mchezo ambao wanatakiwa kushinda kujifariji na kikosi chao bora msimu huu.
Mafanikio ya timu hiyo huyawezi kuyaweka mbali na uwepo wa mchezaji nyota kikosini Alexis Sanchez aliyenunuliwa kwa Euro milion30 ambapo ameonesha thamani yake baada ya kuifungia klabu hiyo magoli 24.
Kwa upande wa kocha Arsene Wenger msimu huu umekuwa bora kwake kushika nafasi ya tatu na kutegemea kucheza fainali ya kombe la FA.
Mategemeo ya msimu ujao kwao ni kuendelea kukitengeneza kikosi cha kupambana katika kampeni ya ubingwa wa England.
Kocha Arsene Wenger anasema wanajiandaa vya kutosha, pia wapo katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na winga wakeTheo Walcott.

0 comments:

Post a Comment