Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa
Monduli. Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa amesema hana rafiki yeyote CCM kwani yeye tayari alishapakia basi la Chadema.
Lowassa amesema ingawa aliwahi kumshauri mgombea ubunge wa jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM, Namelock Sokoine agombee lakini mambo yalivyobadilika alimshauri ajitoe hata hivyo alikataa na hivyo yeye sasa anamuunga mkono mgombea ubunge wa Chadema katika jimbo hilo, Julius Kalanga.
Akizungumza na wananchi wa Lokusale katika mkutano wa kampeni Lowassa alisema, "Suala la ubunge wa Monduli ni kweli nilimshawishi Namelock agombee ubunge lakini mambo yalipobadilika nilimshauri ajitoe, sasa kama CCM hainitaki kwa nini abaki, sina rafiki CCM,"alisema Lowassa na kuongeza: "Kama mtu amebaki CCM mimi nifanye nini? Alihoji Lowassa na wananchi wakijibu "Unamwachaaaaaaaa."
Huku wananchi wakishangilia Lowassa alisema amempendekeza Kalanga hivyo Namelock akubali kwa kuwa mbunge anayefaa Monduli ni Kalanga.
Aliwaambia wananchi hao wamnadi Kalanga kama Mbunge wao na wakiulizwa na mtu yeyote wamjibu kuwa Lowassa ndiye amewatuma.
"Moran mfanye kazi hiyo na pia mlinde kura. Nawapa ushauri wa bure kwamba mbunge anayefaa ni Kalanga kwa ushauri wangu mumchague na mtu asiwasumbue."
Lowassa aliwaambia wananchi hao kuwa akiingia madarakani suala la barabara litashughulikiwa kwani ndicho kitu pekee kinachowapa tabu wananchi wa Lokusale.
Tuesday, 6 October 2015
Lowassa:Sina tena rafiki CCM
Related Posts:
NECTA Yabadilisha Viwango vya Ufaulu Form 6, DIV I Mwisho point 7 NECTA imetoa mwongozo wa matumizi ya viwango vya Ufaulu (Aprili 2014) ambao umesambwazwa katika shule zote ze sekondari kupitia kwa Maafisa Elimu wa Mikoa. Kwa mujibu wa mwongozo huo Madaraja ya ufaulu… Read More
Kashfa nzito Bajeti ya Nishati na Madini Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono wameingia katika mvutano baada ya ujumbe wa maandishi wa kutaka kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kusambazwa kwa wabunge. H… Read More
Ubalozi wa Marekani Kuhamishia Shughuli Zake Tanzania Kutoka Kenya! Serikali ya Marekani imesema itapunguza wafanyakazi katika ubalozi wake nchini Kenya kutokana na kitisho cha ugaidi. Marekani imechukua hatua hiyo baada ya vitisho na mashambulizi ya kigaidi kuzidi kupamba moto nch… Read More
Tundu Lissu: Sheria Gani ilimruhusu Salma Kikwete Kufanya Mkutano wa Siasa Kusini? Mh. Tundu Lissu mbunge na mwanasheria mashuhuri akichangia hoja katika wizara ya mambo ya ndani ameulizia sheria ambayo imemruhusu Salma Kikwete kufanya mikutano ya kisiasa Mtwara wakati jeshi la polisi lilipiga maru… Read More
Bango la Matangazo Barabarani Laangukia Gari Round About Kawe Serikali ipige marufuku makampuni ya kutengeneza Mabango kuweka mabango karibu na Barabara ya wekwe mbali na barabara mita 20 kutoka Barabara kuu hili limeanguka Round about ya Royal Oven njia ya kwenda Lugalo Golf … Read More
0 comments:
Post a Comment