Amini usiamini huku watu wengi Afrika Mashariki wakilazimika kulipa mabilioni ya shilingi ilikujifunza kuendesha magari,teknolojia sasa imepiga hatua moja zaidi.
Mwanzo ilikuwa ni magari madogo sasa kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari Daimler Mercedes-Benz imezindua lori linalojiendesha lenyewe!
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo yenye asili yake nchini Ujerumani,Wolfgang Bernhard alibofya kidude na mara lori likachukua usukani na kuenda lenyewe pasi na kusababisha ajali ya aina yeyote.
Lori hilo linatumia teknolojia ya kamera kwa pamoja na 'radar' kukwepa magari mengine barabarani.
Aidha mtambo huo unatuma na kupokea taarifa na mawasiliano iwapo lori hilo linasogea karibu zaidi kitu chochote iwe ni gari,mti ama hata mtu barabarani.
Hata hivyo kampuni hiyo ilisisitiza kuwa sharti dereva awe hapo wakati wote kifaa hicho cha "highway pilot" kinapotumika kama tahadhari kusitokee ajali.
Lorry hilo aina ya Actross lilijaribiwa katika barabara inayotumika na uma ya Baden-Wurttemberg Ujerumani.
Kwa mujibu wa bwana Bernhard lori hilo lilimudu kujiendesha na hata kutimia kasi ya Kilomita 80 kwa saa.
Mkurugenzi huyo alikuwa na Waziri Winfried Kretschmann walikuwemo ndani ya lori hilo wakati wa jaribio hilo la kihistoria.
Bernhard alissistiza kuwa wakati dereva anapohisi amechoka gari hilo linaweza kuchukua usukani naye ajipumzishe kidogo japo kwa kutengeneza kikombe cha chai huku kamera na mfumo huo wa radar zikidhibiti usukani.
Mfumo huo unatumia miale kubaini kona na maelezo kwenye mabango barabarani.
''Kwa hakika hata uwe mstadi kivipi , mfumo huu wa "highway pilot" unaendesha vyema zaidi kuliko mwanadamu na hata iwe kwa kiwango kipi haiwezi kuchoka sawa na vile madereva wa malori huwa wanawachoka na kupoteza umakinifu barabarani.'' alisema mkurugenzi wa kampuni hiyo Wolfgang Bernhard.
Tuesday, 6 October 2015
Kampuni ya Mercedes yatengeneza Malori yanayojiendesha.
Related Posts:
Watu 29 wauawa msikitini baada ya mlipuaji kujitoa mhanga Nigeria. Watu 29 wameuawa kati mji mkuu wa jimbo la Borno Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua ndani ya msikiti. Kamishna wa polisi katika jimbo la Borno amesema kuwa watu wengine… Read More
BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika kurasa za magazeti yote ya leo Jumatatu,Juni 1. MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuh… Read More
China yaikingia kifua Marekani ujenzi wa baharini. Mmoja wa makamanda wa ngazi za juu katika jeshi la China ametetea hatua ya nchi hiyo za kuokoa ardhi kutoka baharini katika maeneo yanayozozaniwa kusini mwa china. Kauli hiyo inawadia siku moja baada ya Marekani kutaka … Read More
Lori la mafuta laua watu 70 Nigeria.Karibu watu 70 wamefariki huko mashariki mwa Nigeria baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto. Police wanasema huenda kilichosababisha moto huo ni ajali. Walioshuhudia wanasema dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti nd… Read More
Wanaharakati walishutumu jeshi la Iraq Wanaharakati wa haki za binadamu wanalishutumu Jeshi la Iraq kwa kushindwa kuokoa maelfu ya watu kufikia sehemu salama ya nchi hiyo mara baada ya wao kukimbia mapigano katika jimbo la Anbar . Wanaharakati hao wanasema ser… Read More
0 comments:
Post a Comment