Majaji saba wa mahakama ya juu nchi Ghana kati ya 12 wamesimamishwa kazi kwa mda kufuatia madai ya kuhusika katika ufisadi.
Mwezi uliopita majaji wengine 22 wa ngazi za chini walisimamishwa kazi baada ya filamu moja kuwaonyesha wakichukua hongo kutoka kwa wateja ili wapate kupendelewa katika kesi.
Filamu hiyo ilizua hisia kali wakati ilipoonyeshwa mara ya kwanza mjini Accra.
Majaji wengine kadha wamekataa madai hayo na kwenda mahakamani kupinga kusimamishwa kwao kazi.
Saba hao walikuwa na kesi ya utovu wa nidhamu kufuatia makala yaliyoandaliwa na mwandishi Anas Aremeyaw.
Mwandishi huyo anamiliki ukanda wa video wa takribam saa 500 kuhusu ushahidi unaowaonyesha majaji hao wakitaka kupewa hongo.
Majaji wengine 22 wa mahakama ya chini pia wamesimamishwa kazi huku wengine wakikana madai hayo.
Makala hayo ya bwana Anas yamelishtua taifa la Ghana na yameonyeshwa katika majumba ya kuonyeshea filamu katika mji mkuu wa Accra.
Saba hao ni majaji wenye nyadhfa za juu zaidi kusimamishwa kazi nchini humo.
Jaji mkuu Goergina Theodora Wood ameanzisha kesi dhidi yao kulingana na baraza la majaji nchini humo.
Uchunguzi pia utafanywa ili kubaini iwapo wana hatia au la.
Tuesday, 6 October 2015
Majaji 7 wasimamishwa kazi kwa Ufusadi Ghana.
Related Posts:
Mmiliki wa Kampuni ya ALIBABA ndiye anaeongoza kwa utajiri nchini China.Mwanzilishi wa mtandao wa Alibaba ndiye tajiri mkubwa zaidi nchini Uchina kulingana na rekodi za kampuni yake. Hili imethibitishwa na ripoti rasmi ya kifedha ya Hurun. Bw.Ma ameongoza orodha ya watu tajiri zaidi nchini Uchina… Read More
Wanafunzi 12,000 wakosa nafasi Vyuo vikuu,TCU yawapa nafasi ya Pili.Wanafunzi 12, 000 wakosa nafasi za vyuo vikuu, TCU yawapa nafasi ya pili kuchagua nafasi za masomo (course) ambazo bado ziko wazi na wameshauriwa kutochagua "course" zenye ushindani mwingi maana hii itasababisha wengine kukos… Read More
Mtanzania ateuliwa kuwa makamu mkuu wa Rais wa BET Networks. BET Networks, ambayo ipo chini ya kampuni ya Viacom Inc. imetangaza kumwajiri Kay Madati kama makamu mkuu wa rais (Executive Vice President) na pia kama Chief Digital Officer. Madati, raia wa Tanzania aliyeishi katik… Read More
Hoteli iliyojengwa katikati ya Maji huko SpitBank Fort-Uingereza miaka 134 iliyopita. HOTELI ya Spitbank Fort ikionekana kwa juu ikiwa imejengwa mwaka 1879 katikati ya kina maji ya habari nchini Uingereza ikiwa na umri wa miaka 134. Hapa ikionekana katikati ya kina cha maji ya b… Read More
Viwanja vya ndege vilivyo "busy" zaidi duniani. Wakati nchi kama Tanzania inapambana kujenga viwanja vya ndege ili ndege kubwa kama za Fastjet ziweze kutua sehemu kama Musoma, Kigoma na Arusha baada ya kuweza kufanya safari zake kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Mb… Read More
0 comments:
Post a Comment