Facebook

Monday 25 January 2016

Hizi ni tetesi zote za Usajili wa wachezaji barani Ulaya siku ya leo J'Tatu.

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal,
64, anakaribia kujiuzulu baada ya kukiri kuwa
amewaangusha mashabiki (Sun), Van Gaal
atakuwa na mazungumzo na makamu mwenyekiti wa United Ed Woodard kujadili jinsi ya kukatisha
mkataba wake unaokwenda hadi mwaka 2017
(Star), Woodward amezungumza na wachezaji
wakuu wa United kuhusiana na mikakati ya Van Gaal na anafikiria kumteua Ryan Giggs kuwa meneja hadi mwisho wa msimu (Mail), meneja wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho, 52, anazidi kupata matumaini ya kuwa meneja wa Manchester United (Times),

Meneja wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anaamini
Manchester United wangekuwa tayari wamempa
kazi Jose Morinho, kama wangekuwa wanamtaka,
na anadhani wanasubiri hadi mwisho wa msimu
kujaribu kumchukua meneja wa Bayern Munich,
Pep Guardiola, 45, au Diego Simione, 45 kutoka
Atletico Madrid (Telegraph),

Liverpool wamekubaliana maslahi binafsi na Shaktar
Donetsk, kumsajili mshambuliaji Alex teixeira, 26
(Futbol Ukraine), hata hivyo bado hakuna
muafaka juu ya ada wanayotaka kutoa Liverpool
na bei iliyowekwa kwa mchezaji huyo kutoka
Brazil (Liverpool Echo),

Kiungo wa Fiorentina
Mario Suarez anafikiria kuhamia Watford (Mirror),

Roma wamethibitisha kuwa wanazungumza na
Jiangtsu Suning ya China kuhusiana na kumuuza
mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho,
28 (Guardian),

Mshambuliaji wa Atletico Madrid
Antoine Greizman, 24, amesema hana mpango
wa kuondoka Spain na kujiunga na Chelsea kwa
pauni milioni 75 (Telefoot),

Chelsea wamekuwa
wakimalizia kukamilisha usajili wa Alexandre
Pato, 26, kutoka Corinthians kwa mkopo, huku
wakitazamia kumsajili moja kwa moja baadaye
(Mail),

Newcastle wamepunguza kasi ya
kumnyatia winga wa Tottenham Andros
Townsend, 24 kutokana na Spurs kutaka pauni
milioni 14 (Sky Sports),

Newcastle wanaonekana
kufanikiwa kubaki na kiungo kutoka Ufaransa,
Moussa Sissoko, 26, lakini mchezaji huyo
amesema huenda akaondoka mwisho wa msimu (Sun),

Mshambuliaji wa Liverpool Christian
Benteke, 25, huenda akaondoka Anfield baada ya michuano ya Euro 2016 (Bleacher Report),

Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany, 29, anakabiliwa na jeraha jingine la msuli wa mguu na huenda asicheze kwa mwezi mmoja zaidi (Star).

Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa
kwenye magazeti ya leo Ulaya. Tetesi nyingine
kesho tukijaaliwa. Zimesalia siku saba kabla ya
dirisha hili la usajili kufungwa.

www.bantuz.com

0 comments:

Post a Comment