Facebook

Saturday 19 September 2015

Bacary Sagna aeleza sababu ya kunyoa rasta zake.

Bacary Sagna alikua anatambulika kirahisi kwa rasta zake ambazo zilikua na rangi. Sasa akiwa kwenye mapumziko ya likizo baada ya msimu uliopita alinyoa rasta zake na picha yake kusambaa sana kwenye mtandao ya kijamii.

Sasa akiwa kwenye kipindi cha maswali na majibu katika Manchester City Tv, moja ya swali lililoulizwa na mashabiki wengi ni kuhusu kwanini amenyoa rasta zake.

Jibu lake ni kwamba yeye binafsi alikua na mpango wa kuzinyoa muda wowote, lakini sababu ya msingi iliyomfanya anyoe zile rasta ni sherehe ya asili aliyoshiriki kwao Senegal ambayo ilikua lazima anyoe nywere zake.

0 comments:

Post a Comment