Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Friday, 10 April 2015

MGOMO WA MADEREVA WAMALIZWA SALAMA DSM

Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa
kumaliza mgomo wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo
lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma
tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)
Kuhusu suala la Madereva kusoma, Serikali na Madereva
wamekubaliana kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia
mbadala

Ronaldo azidi kuvunja rekodi Real Madrid.

Cristiano Ronaldo ametimiza idadi ya magoli 300 katika mechi 288 -
sasa amebakiza magoli 23 kumfikia Raul Gonzales Blanco - Je
ataifikia rekodi hiyo msimu huu au msimu ujao?

CHELSEA YAMNYATIA MSHAMBULIAJI HATARI WA KIJAPAN,MUTO

Chelsea wametangaza dau kutaka kumsajili mchezaji wa kimataifa
kutoka Japan Yoshinori Muto. Shirika la habari la Japan, Kyodo
limesema mchezaji huyo wa klabu ya FC Tokyo bado hajaamua kama
anataka kuhamia Stamford Bridge au la msimu ujao.

Muto, 22,
amechezea timu ya taifa mara 11 na amepachika mabao matatu
katika mechi nne za mwanzo wa msimu mpya wa ligi ya Japan, J-
League. Msimu uliopita alifunga mabao 13 na alitajwa katika kikosi
cha taifa kilichocheza hadi robo fainali ya kombe la Asia. Aliitwa
tena na kocha mpya Vahid Halilhodzic katika mechi yake ya kwanza
mwezi uliopita.

Muto alifuzu shahada ya uchumi katika chuo kikuu cha
Keio wiki mbili zilizopita. Mwezi Februari, Chelsea walitangaza
mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya kutengeneza matairi ya
Japan wenye thamani ya pauni milioni 40 kwa mwaka.

Frank Ribery amponda Van Gaal.

Franck Ribery amtaja kocha Louis Van gaal kama "mtu mbaya(bad
man)
Franck Ribery hajaogopa kutoa maoni yake juu ya kocha Louis Van
Gaa,huku akitoa siri ya mausiano yaliyo kuwa na sumu kati yao alipo
kua katika klabu ya Bayern Munich 2009-2011
Franck Ribery alimbandika jina Luis Van Gaal kama "mtu mbaya" na
kusema uongozi wa kocha huyo raia wa Uholanzi katika klabu ya
Bayern Munich kuli mlazimisha yeye kutaka kufikilia kuhama timu

"tulikuwa na kutokuelewana linapo kuja katika swala la
ubinadamu.alipokua anaanza hakuna aliekuwa anajua nini kitakuja
kutokea" alisema mshambuliaji raia wa ufaransa
"wazo lake lilikuwa nikwamba alikuwa hajali kuhusu majina hata
kidogo,huitaji mastaa,kila mtu alitakiwa ajionyeshe na kumthibitishia
upya tena

"kwa mara ya kwanza nakutana nae ilikuwa tayari nimesha pewa
sumu.kama mchezaji wa kulipwa unapoteza imani.anafanya mambo
makubwa uwanjani lakini kocha Van Gaal alikua mtu
mbaya.Mahusiano yetu yali vunjika"

Ribery slifunga magoli 7 tu,msimu wake mbaya zaidi baada ya
kurejea akiwa chini ya Van Gaal katika msimu wa kwanza,huku
akitakiwa kutafuta mlingano na mchezaji mpya Arjen Robben,Ribery
alipata wakati mgumu mbako kulipelekea yeye kutaka kuondoka
Bayern "ulikua ni mzigo" alisema

"klabu nyingi zili jaribu kunishawishi ni badilike;Real Madrid,Barcelon
a,Juventus,Chelsea,Manchester City.unaanza kufikilia,nilifanya
maamuzi yangu juu ya wapi nataka ni jengee maisha yangu ya
kisoka.Nadhani huu ndio utu"

Ronaldo afutiwa kadi ya njano kwa kosa la kujiangusha.

Cristiano Ronaldo sasa ataweza kuichezea Real Madrid vs Elbar
wikiendi hii, baada ya kadi ya njano aliyoonyeshwa kwa kosa la
kujirusha kufutwa

HUU NDIO UZI MPYA WA LIVERPOOL FC

Raheem Sterling ambaye wiki iliyopita alikataa
mkataba wa kulipwa mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki Liverpool-
anaonekana hapa na wachezaji wenzake Martin Skirtel, Simon
Mignolet na Daniel Sturridge, wakionesha jezi mpya watakazovaa
msimu ujao. Jezi hizo zimezinduliwa siku ya Ijumaa.

IBRAHIMOVIC AFUNGIWA MECHI NNE

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic
amefungiwa kucheza mechi nne za ligi kuu ya Ufaransa baada ya
kunaswa na picha za televisheni akitukana.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Sweden alikasirika na
kuwashutumu waamuzi na pia kutukana baada ya timu yake kupoteza
3-2 dhidi ya Bordeaux mwezi uliopita. Ibrahimovic, 33, baadaye
aliomba radhi na kusema matamshi yake

"hayakuwa yamelenga
Ufaransa au wananchi wake".
Atakosa mechi nne kati ya saba zilizosalia za ligi. Kamati ya nidhamu
ilisema adhabu hiyo imezingatia "aina ya kosa na uzito wa matamshi
yake".

Ibrahimovic pia atakosa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya
Champions League dhidi ya Barcelona kufuatia kadi nyekundu
aliyopewa katika mchezo uliopita dhidi ya Chelsea. Hata hivyo
ataweza kucheza mechi ya fainali ya kombe la ligi siku ya Jumamosi
dhidi ya Bastia.

Wednesday, 8 April 2015

"NAONGEA NA BRENDAN RODGERS"

Nawaza eti hivi Liverpool inahitaji nini ili imalizie pale ilipoishia msimu uliopita achana na msimu huu labda hata ujao.

Je inakosa nini kinachoizuia kwenda mbele!!! NI sahihi kutoka nafasi ya pili hadi yatano na saba!!? Ni kweli kuondoka kwa Suarez ndiko kulikorejesha machungu Anfield!!?

JE unaweza ukawa mwanzo wa miaka mingine mingine mingi ya kutoishuhudia Liverpool katika ligi ya Mabingwa!!!?

Bado nina maswali mengi ya kujiuliza ila akili yangu inaamini Rodgers ndie aliefanya kuondoka kwa Suarez kuwa ndo sumu ya kuitafuna Liverpool

Liverpool ilikuwa imekamilika kila idara siamini kama kuondoka kwa Suarez ilikuwa ndo sahihi kwa Liverpool kupata matokeo haya.

Katika kikosi cha msimu uliopita ni Suarez pakee alieondoka katika timu ya dhahabu iliyonyimwa ubingwa na "upumbavu" wa Gerrard

Sidhani kama ilikuwa sahihi kwa Rodgers kuchanganyikiwa baada ya kuthibitika Suarez anaondoka,Rodgers alichanganyikiwa aliona kuondoka kwa Suarez ni sawa na kuondoka kwa wachezaji 8 hivi ndo mana akaingia sokoni kununua wachezaji bila kuangalia mahitaji ya timu.

Alikuwa ni sawa na mtu aliepoteza jino moja na kuamua kununua bandia 8 kisha akayang`oa na mengine nane ya zamani na kuweka bandia!!!!?

Aliivuruga timu yake yote hasa kikosi cha kwanza, harafu bahati mbaya kwake hakuna mchezaji anaeweza kucheza game 3 mfululizo katika ubora unaostahili

Coutinho wa jana si wa game ya kesho, kiungo kibovu na kosa kubwa analofanya ni kutokuwa na Mfungaji ila ana wapaka rangi Sterling na Sturridge

Sijui kwanini haiamini miguu ya Mario Balloteli au anadhani ataibuka tu ghafla!!! Ilikuwa ni lazima aendelee kumpa nafasi angezoea tu

Je kwasasa anataka nini tena Anfield!!?

JE ana uwezo wa kufikia mafanikio hata ya msimu uliopita,alisajili wachezaji zaidi ya 8

JE NI BORA KULIKO ALIOKUWA NAO ?

Nahisi kama UWEZO WAKE KWA LIVERPOOL umefikia mwisho ila ni Meneja mzuri lakini hakuna atakachokipata Liverpool.

Imeandaliwa na Emmanuel Noel.