Facebook

Wednesday 8 April 2015

"NAONGEA NA BRENDAN RODGERS"

Nawaza eti hivi Liverpool inahitaji nini ili imalizie pale ilipoishia msimu uliopita achana na msimu huu labda hata ujao.

Je inakosa nini kinachoizuia kwenda mbele!!! NI sahihi kutoka nafasi ya pili hadi yatano na saba!!? Ni kweli kuondoka kwa Suarez ndiko kulikorejesha machungu Anfield!!?

JE unaweza ukawa mwanzo wa miaka mingine mingine mingi ya kutoishuhudia Liverpool katika ligi ya Mabingwa!!!?

Bado nina maswali mengi ya kujiuliza ila akili yangu inaamini Rodgers ndie aliefanya kuondoka kwa Suarez kuwa ndo sumu ya kuitafuna Liverpool

Liverpool ilikuwa imekamilika kila idara siamini kama kuondoka kwa Suarez ilikuwa ndo sahihi kwa Liverpool kupata matokeo haya.

Katika kikosi cha msimu uliopita ni Suarez pakee alieondoka katika timu ya dhahabu iliyonyimwa ubingwa na "upumbavu" wa Gerrard

Sidhani kama ilikuwa sahihi kwa Rodgers kuchanganyikiwa baada ya kuthibitika Suarez anaondoka,Rodgers alichanganyikiwa aliona kuondoka kwa Suarez ni sawa na kuondoka kwa wachezaji 8 hivi ndo mana akaingia sokoni kununua wachezaji bila kuangalia mahitaji ya timu.

Alikuwa ni sawa na mtu aliepoteza jino moja na kuamua kununua bandia 8 kisha akayang`oa na mengine nane ya zamani na kuweka bandia!!!!?

Aliivuruga timu yake yote hasa kikosi cha kwanza, harafu bahati mbaya kwake hakuna mchezaji anaeweza kucheza game 3 mfululizo katika ubora unaostahili

Coutinho wa jana si wa game ya kesho, kiungo kibovu na kosa kubwa analofanya ni kutokuwa na Mfungaji ila ana wapaka rangi Sterling na Sturridge

Sijui kwanini haiamini miguu ya Mario Balloteli au anadhani ataibuka tu ghafla!!! Ilikuwa ni lazima aendelee kumpa nafasi angezoea tu

Je kwasasa anataka nini tena Anfield!!?

JE ana uwezo wa kufikia mafanikio hata ya msimu uliopita,alisajili wachezaji zaidi ya 8

JE NI BORA KULIKO ALIOKUWA NAO ?

Nahisi kama UWEZO WAKE KWA LIVERPOOL umefikia mwisho ila ni Meneja mzuri lakini hakuna atakachokipata Liverpool.

Imeandaliwa na Emmanuel Noel.

0 comments:

Post a Comment