Facebook

Friday 10 April 2015

IBRAHIMOVIC AFUNGIWA MECHI NNE

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic
amefungiwa kucheza mechi nne za ligi kuu ya Ufaransa baada ya
kunaswa na picha za televisheni akitukana.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Sweden alikasirika na
kuwashutumu waamuzi na pia kutukana baada ya timu yake kupoteza
3-2 dhidi ya Bordeaux mwezi uliopita. Ibrahimovic, 33, baadaye
aliomba radhi na kusema matamshi yake

"hayakuwa yamelenga
Ufaransa au wananchi wake".
Atakosa mechi nne kati ya saba zilizosalia za ligi. Kamati ya nidhamu
ilisema adhabu hiyo imezingatia "aina ya kosa na uzito wa matamshi
yake".

Ibrahimovic pia atakosa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya
Champions League dhidi ya Barcelona kufuatia kadi nyekundu
aliyopewa katika mchezo uliopita dhidi ya Chelsea. Hata hivyo
ataweza kucheza mechi ya fainali ya kombe la ligi siku ya Jumamosi
dhidi ya Bastia.

0 comments:

Post a Comment