Facebook

Friday 10 April 2015

CHELSEA YAMNYATIA MSHAMBULIAJI HATARI WA KIJAPAN,MUTO

Chelsea wametangaza dau kutaka kumsajili mchezaji wa kimataifa
kutoka Japan Yoshinori Muto. Shirika la habari la Japan, Kyodo
limesema mchezaji huyo wa klabu ya FC Tokyo bado hajaamua kama
anataka kuhamia Stamford Bridge au la msimu ujao.

Muto, 22,
amechezea timu ya taifa mara 11 na amepachika mabao matatu
katika mechi nne za mwanzo wa msimu mpya wa ligi ya Japan, J-
League. Msimu uliopita alifunga mabao 13 na alitajwa katika kikosi
cha taifa kilichocheza hadi robo fainali ya kombe la Asia. Aliitwa
tena na kocha mpya Vahid Halilhodzic katika mechi yake ya kwanza
mwezi uliopita.

Muto alifuzu shahada ya uchumi katika chuo kikuu cha
Keio wiki mbili zilizopita. Mwezi Februari, Chelsea walitangaza
mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya kutengeneza matairi ya
Japan wenye thamani ya pauni milioni 40 kwa mwaka.

0 comments:

Post a Comment