Zaidi ya watu miatatu bado hawajapatikana baada ya meli iliyokuwa imewabeba wanafunzi kuzama nchini Korea Kusini.
Awali maafisa walikuwa wamesema kuwa wengi wa abiria waliokuwa katika meli hiyo waliokolewa."Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikaanza kuegemea upande mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.
"watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."
Bado haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika ajali hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha.
Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu hawajulikani walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.
Watu wawili wamefahamika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne wameokolewa.
Wengi wa abiria wa meli hiyo walikuwa wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya masomo kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.
Meli hiyo ilikuwa na watu 460. Zaidi ya miatatu hawajapatikana , wengine 164 wameokolewa na wengine wawili wamethibitishwa kufariki.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kufahamu kila kinachojiri kuhusu Meli iliyozama Korea Kusini.............
0 comments:
Post a Comment