Facebook

Thursday, 17 April 2014

Fahamu ujumbe wa wanafunzi waliowatumia wazazi wao kabla meli haijazama Korea Kusini......soma hapa....


Takriban watu 300 wakiwa bado hawajapatikana, siku moja baada ya ajali, ripoti za ujumbe wa simu uliotumwa na wale waliokuwa wamekwama ndani ya meli hiyo zimeibuka kupitia vyombo vya habari nchini humo.

Mwanafunzi:"huenda hii ndio mara yangu ya mwisho kukuambia kuwa nakupenda,'' ndio ulikuwa ujumbe wa mwanafunzi mmoja kwa jina Shin Young-Jin kwa mamake.

Kulingana na jarida la Herald nchini humo, Shin alikuwa miongoni mwa watu 179 waliookolewa.
Lakini wazazi wengine waliopokea ujumbe kama huo bado hawajaweza kupatana na watoto wao.

 
Baadhi ya wazazi hawajaweza kuwapata watoto wao


Mawasiliano mengine kati ya mwanafunzi mmoja na babake , yalinukuliwa na shirika la habari la AFP.
Mwanafunzi: "baba usijali, nimevaa boya la kujiokoa na niko na wasichana wenzangu. Tuko ndani ya meli na bado hatujaanza kuokolewa.''
Baba: Najua msaada uko njiani , lakini kwa nini hamjaanza kuelea, tafadhali jaribu kuondoka ndani ya meli kama unaweza.''
Mwanafunzi: ''Kuna msongamano mkubwa na meli tayari imeanza kuzama''
Mwanafunzi aliyetuma ujumbe huu bado hajapatikana.
Familia za abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo walijawa na hisia wakisubiri taarifa zozote kuhusu wapendwa wao.

Abiria walishauriwa kutulia wakisubiri msaada
Katika ujumbe mwingine wa simu, mwanafuzni mmoja alimtumia ujumbe kakake mkubwa meli ilipoanza kuzama.
Mwanafunzi: "meli imekwama na haisongi walinzi wa baharini wameanza kuwasili kujua hitilafu imetokana na nini'
Kakake:'' usiwe na wasiwasi. Fanya kila mnachoamrishwa kufanya na kila kitu kitakuwa shwari.''
Lakini hapakuwa na mawasiliano mengine baada ya hapo.
Baadhi ya wazazi waliweza kuendelea kuwasiliana na watoto wao, hadi mawasiliano yalipokatika.

0 comments:

Post a Comment