Uchunguzi wa kimsingi umebaini.
Waokoaji wamefaulu kuingia ndani ya feri iliyozama.Naibu wa tatu wa nahodha wa ferri iliyozama ''Sewol'' ndiye aliyekuwa usukani wakati feri hiyo ilipozama.
Kiongozi wa Mashtaka ya umma nchini Korea bwana Park Jae-Eok amesema kuwa nahodha mkuu Lee Joon-seok,atakuwa na swali la kujibu .
Watu 26 pekee ndio wamedhibitishwa kufariki kufikia sasa, huku 179 wakiokolewa.
Makundi ya waokoaji wamefanikiwa kuingia ndani ya feri hiyo kwa mara ya kwanza leo asubuhi baaha ya kutoboa shimo upande wa juu wa chombo hicho kilichozama.
Waokoaji walikuwa wameshindwa kuingia ndani ya feri hiyo baada ya bahari kuchafuka.
Mamia ya jamaa na marafiki ya wahasiriwa wamelalamikia ukosefu wa habari za uokaji .
Wengi wamekuwa wakivumilia hali mbaya ya hewa wakiomba kuruhusiwa kusubiri wapendwa wao ufukweni.
Endelea lutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na meli iliyozama Korea kusini kwa wakati muafaka.
0 comments:
Post a Comment