Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa Serikali za
tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia
kikao
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa Serikali za tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao
Wajumbe karibu wote wa vyama vya upinzani wanaoshiriki Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, wametoka nje ya kikao cha leo jioni, wakipinga kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye wajumbe wengi ndani ya bunge hilo, kuwaburuza.
Wakati
akitoa mchango wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
aliliambia Bunge kuwa wanashangazwa na kitendo cha CCM kutaka kutumia
wingi wao, kutengeneza katiba ambayo hailingani na mawazo ya wananchi,
kama yalivyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
Alisema
kitendo kilichofanywa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, William
Lukuvi, kwenda katika kanisa na kusema wanaotaka muundo wa serikali tatu
wanataka kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kiislamu ni uchochezi unaoweza
kuligawa taifa na hata kusababisha machafuko.
Alisema pia wanashangazwa na Rais Kikwete kupokea na kusaini rasimu hiyo, lakini akaja bungeni na kuipinga kwa nguvu kubwa.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata kila kinachojiri katika Vikao vya Bunge la Katiba Mpya
0 comments:
Post a Comment