Mwanaume aliyemuua kwa kumkata kichwa mpenzi wake amepatikana na hatia
ya mauaji nchini Uingereza
Aras Hussein alimkata kichwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 Reema
Ramzan nyumbani kwake katika mtaa wa Sheffield mwezi Juni kabla ya yeye
mwenyewe kujidunga kisu kifuani mwake.
Aras amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Hussein, alikiri kumuua mpenzi wake baada ya kuzozana ingawa awali
alikana madai ya mauaji.
Mwili wa Ramzan ulipatikana katika sehemu ya jikoni ya nyumba ya Hussein
tarehe nne mwezi Juni.
Polisi walipigiwa simu na mpita njia mmoja aliyemuona Hussein akitembea
uchi nje akiwa na damu katika mwili wake.
Madaktari walipojaribu kumsaidia kwa kumpa huduma ya dharura aliwauliza
kwa nini walikuwa wanataka kumsaidia wakati amemuua mtu nyumbani kwake.
Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo, akajibu kuwa hajui.
Mahakama ilisikia ambavyo msichana huyo alidungwa kisu kifuani na kisha
kukatwa kichwa chake.
Pia mikono yake ilikuwa na alama za kuonyesha kuwa alijaribu kujikinga
kutokana na kushambuliwa na mpenzi wake
Kiongozi wa mashitaka aliambia mahakama kuwa marehemu Ramzan bado
alikuwa hai wakati Aras alipoanza kumkata koo kwa kutumia nguvu.
Wakati kesi ilipokuwa inaendelea , mahakama iliambiwa na familia ya
Ramzan kuwa hawakupenda uhusiano kati ya wawili hao.
Siku ya kuuliwa kwake, alikuwa amekwenda nyumbani kwa Aras akiwa na Pasi
yake ya usafiri pamoja na kitita kikubwa cha pesa.
Chanzo
0 comments:
Post a Comment