Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa shule ya mabweni
ya wasichana imeshambuliwa katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa
nchi hiyo huku wasichana wakitekwa nyara.
Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili wametekwa nyara na washambuliaji hao.Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi wawili waliuawa huku mali ikiharibiwa wakati wa shamblizi hilo mjini Chibok.
Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi ya watu 70, waliuawa katika milipuko miwili ya mabomu katika kituo cha mabasi mjini Abuja.
Kundi la Boko Haram pia limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo.
0 comments:
Post a Comment