Facebook

Friday, 18 April 2014

Upinzani Watoa Tamko lao leo kuhusu kugomea Vikao Vya Bunge....soma soma kauli zao mbalimbali hapa......


Screen Shot 2014-04-17 at 4.50.42 PM
Baada ya kugoma na kuamua kutoka nje ya bunge la katiba Dodoma  kikundi cha umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) kimekutana na waandishi wa habari April 17 2014 na kuyazungumza haya yanayofata hapa chini.
 
                                         Profesa Ibrahim Lipumba 
  ‘Tumekubaliana kwamba siku ya Jumamosi kwa pamoja Wabunge wote ambao hatuna dharura tutakua tumekwenda Zanzibar kwenye mkutano wa hadhara kuanzia saa nne asubuhi, tutaondoka na boti asubuhi saa moja kuelekea Zanzibar na tutaeleza yaliyojiri katika bunge hili maalum’‘Baada ya hapo tutaendelea na mikutano nchi nzima kujulisha Wananchi msimamo wetu ambao ni rahisi, uko wazi kwamba Rais aliunda tume ya katiba katika utaratibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba itayokusanya maoni ya Wananchi lakini katika yale mapendekezo ambayo yamekuja ukawa ni mjadala wa matusi, kejeli, lugha za kibaguzi na kutaja Wapemba, Waarabu, Wakongo na Wahindi, viongozi wapo na hamna aliewakanya tena ndio wanawapigia makofi

Freeman Mbowe
  ‘Tume iliundwa kuratibu zoezi kupata mawazo ya Wananchi kufanya utafiti ambao uliipa tume rejea maalum ya kufata, tume haikukusanya tu maoni ya Wananchi bali ilifanya pia tafiti nyingi na ilikua na timu kubwa tu ya watu makini na mahiri na ikaonekana muafaka wa muungano wa kudumu ni serikali tatu’
‘Kinachofanyika pale bungeni ni kutulazimisha kuondoka kwenye msingi wa ile rasimu na kuzusha rasimu mpya ambayo inapendekeza mfumo wa serikali mbili, mfumo ambao haujafanyiwa utafiti na haujatolewa maoni na Wananchi, je tumeletewa nyaraka za kutosha za kujadili serikali mbili?’
Screen Shot 2014-04-17 at 4.49.07 PM
‘Ni dhahiri kama tunataka kuvunja ule msingi wa rasimu iliyoletwa na Warioba turudi kutengeneza rasimu nyingine ambayo ina mfumo wanaopendekeza wao lakini hatuwezi kupitia mgongo wa tume ya Warioba kwenye msingi wa rasimu iliyoletwa ya serikali tatu alafu tukajadili mfumo wa serikali mbili, hata wajumbe hawana mamlaka hayo’

‘Hatuwezi kushiriki katika majadiliano yenye matusi, kejeli, dharau na kupotosha umma…. kauli zinatolewa na viongozi zinapindishwa, wabunge wa upande wetu wakitoa mawazo yao na kueleza ukweli… unageuzwa kuwa karaha, kututaka sisi tuendelee kushiriki katika udhalilishaji ule hakika hatuwezi… je tutapata tutakachokitaka?
‘Kuna njia nyingi za kuitafuta haki, haki inaweza kutafutwa ndani ya bunge au nje ya bunge, kazi yetu kama vyama vya siasa ni kuweka shinikizo na kujenga hoja za shinikizo, kama tumeshapeleka maoni yetu hayaheshimiwi huna busara yoyote unaweza kutumia kwenye genge la watu kama wale ambao wamekaririshwa maneno’
‘Wao wanatulaumu sisi UKAWA tunakaa tunaweka misimamo lakini wao wanakuja ndani ya bunge kujadili mambo ambayo wamejadili wao, na wanajadili Waziri mkuu akiwa miongoni mwao’ 
 
Endelea kufuatilia kila kinachojiri Dodoma kwa kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari kamili kwa muda muafaka

0 comments:

Post a Comment