Unaweza
ukadhani ni ndoto lakini hii ni habari ya kweli baada ya Hifadhi ya
jamii NSSF kutangaza uwezekano wa kujengwa daraja la kihistoria zaidi
litakalounganisha Dar es salaam na Zanzibar.
Uwepo
wa daraja hilo unaweza kuwa ni neema kwa Watanzania wote na hata nchi
za jirani kwani itarahisisha shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa
asilimia kubwa kwa kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi.
Gazeti
la HabariLEO liliripoti kuwa kwa sasa Shirika hilo lipo katika
mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga
daraja hilo katika bandari ya Dar kwa upande wa Bara na Unguja kwa
upande wa Visiwani.
Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ramadhan Dau alisema
ujenzi wa daraja hilo si ndoto bali ni ukweli na tayari wameanza
mazungumzo ya awali ili kutimiza malengo yao.
Umbali kati ya Dar
na Zanzibar ni kilometa73.43 sawa na maili45.62 hivyo kuwepo na mradi
huo ni jambo linalowezekana kwani kuna madaraja marefu zaidi duniani
yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.
Kwa sasa
daraja refu zaidi duniani kote ni lile la Danyang-Kushan lililopo nchini
China ambalo lina umbali wa kilometa 165 sawa na maili102.4 ambalo
lilifunguliwa Juni mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment