Facebook

Wednesday, 5 November 2014

Utambue ujangiri unaofanywa kupitia akaunti za facebook


Habari zenu wadau wa BantuTz... Mataifa hivi sasa yanapambana vikali na CYBER CRIME ambapo hivi karibuni IRAN wamevipiga vyombo vya usalama vya MAREKANI attack kwa computers ambazo zinakuwa kwa ajili ya Ulinzi na Usalama wa systems mbali mbali zinazoongozwa na computers kama vile RADAR na vinginevyo hii imekuwa hali ya hatari...Na leo BantuTz tumeona ni bora tushirikishane nanyi juu ya security system ambayo wengi huwa hatujui....Ushawahi kuona Page inaonesha FACEBOOK afu ukiangalia web address unaona mfano www.katemimethsela.net/facebookingnow Huu ni mfano tu sio kwamba ndio web halisi....

TAZAMA MIFANO HII KWANZA...ANGALIA PAGE NA URL YAKE JUU HAPO





SASA NADHANI UNAWEZA JUA NINI SOMO LETU LEO COMPLEX HAPA EEH??

Sasa kuna moja ambayo ni Hatari zaidi ambayo wengi huwa wanaiogopa sana ebu itazame hii....



TUANZE UPEMBUZI WETU HALISI WA LEO KAMA HIVI

Wana complex Leo nlipenda tushirikishane mtandao mmoja hivi ambao wametengeneza webiste kwa lengo la ku HACK ACCOUNT za watu Facebook kwa kujidai wanataka sapot yako katika kuLIKE picha zao ama wanataka uCOMMENT....Hichi kitendo huitwa PHISHING??

PHISHING ni NINI???



Phishing kwa maana ya Rahisi na ya Haraka ni ku-LEGITIMIZE (kuhalalisha) mtandao Feki na kuchukua informations mbali mbali za watu kwenye mtandao halali kabisa na baada ya hapo kwa lengo la ku HACK na kuchukua informations....Huu mfumo mtu huchukua mwonekano halisi wa website anayoitaka na kuweka picha na rangi kama zile lakn tofauti inakuja kwenye mwonekano wa WEB ADDRESS (URL)

Kwa mfumo huu hacker anaweza ku-PROMPT na kukutaka User uingize details za mtandao huo Fake wakati wewe ukidhani ni mtandao halisi....Japo kwa ufupi naamini tunaenda sawa hapo.

ENHEE MTANDAO UPI LEO UNAWEKWA KATI
Kwa siku ya Leo wadau wa BantuTz Nimeona niwashirikishe juu ya mtandao huu wakijangili unaofanana na FACEBOOK wakat sio REAL FACEBOOK....

TAHADHARI: Usibonyeze hii link kama bado umeLOGIN facebook huo ni mtandao hatari sana wa majangili

Mtandao huo unaitwa www.facebook-team.wapka.mobi/

HAKIKISHA UMELOGOUT FACEBOOK NDO UCHEKI HYO LINK....Kwa wale ambao wangependa waone nini kinaonekana kwenye hyo link Complex Tunakupa kama hivi...



UPEMBUZI YAKINIFU KUJUA UHALALI WA MTANDAO HUO
Mtandao huo kwanza hauonekani location yake hasa iko wap, Kwa uchunguzi nliofanya nimefanikiwa kugundua tu IP address ya mtandao huo kama ripoti hapo chini inavyoonesha


haka.jpg


Na hii pia wakati nikiwa na TRACE ROUTE

haka1.jpg


USHAURI NA MAPENDEKEZO
Hakikisha akaunt yako ya FaceBook inamuonekano kama huu kule kwenye settings



Kama mtumizi salama wa computer jitahidi kuepuka kutembelea sites za ajabu ajabu ambazo huzielewi elewi, hazina mawasiliano ya haraka kama VALID PHONE NUMBERS, na Pia epuka kuangalia links ambazo zinakuambia kuingize details zako za Facebook.....Kama utakuwa na Swali karibu sana, kama una chochote cha kuongezea na mengine mengi karibuni.
 
Imeandaliwa na Katemi Methsela

0 comments:

Post a Comment