Facebook

Wednesday 18 November 2015

Bomoa bomoa yaikumba Wilaya ya Kinondoni leo.

Hizi ni baadhi ya picha za bomoa bomoa katika eneo la tukio hapa Mwenge, baada ya hapo wameenda katika maeneo menginie ikiwemo Tegeta.

Inaelezwa kwamba wakazi waliokuwa wanaishi katika eneo la hilo walitakiwa kuondoka mapema kwa amri ya Serikali kutokana na kwamba maeneo hayo sio sehemu rasmi kwa makazi hivyo nyumba zote zilizokuwa zimewekewa alama ya mkasi zimebomolewa.

Zoezi hili ni muendelezo wa bomoa bomoa katika maeneo yatakayohusika na ubomoaji huo ikiwa ni pamoja na maeneo ya Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni eneo la Biafra.


Baadhi ya majengo yaliyokuwa na maduka yamebomolewa.
Zoezi hilo likiendelea katika eneo la Mwenge.

Baadhi ya Askari wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi wakati wa bomoa bomoa

Kinondoni kuanza bomoabomoa leo

MANISPAA ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo inaanza ubomoaji wa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
Kamishna wa Ardhi wizarani hapo, Moses Kusiluka aliwaambia waandishi wa habari kwamba maeneo yatakayohusika na ubomoaji huo ni Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni eneo la Biafra. “Ubomoaji huu unatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Jumatano (leo) Novemba 18 hadi Ijumaa Novemba 20 mwaka huu,” alisema.
Alisema ubomoaji huo utahusisha nyumba zote zilizojengwa bila kibali cha ujenzi, bila kufuata michoro ya mipango miji na bila kufuata matumizi ya ardhi ambayo ni maeneo ya wazi.
Kamishna huyo alisema ubomoaji huo unafanywa baada ya kubaini kuwa maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma yamekuwa yakitumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.

0 comments:

Post a Comment