Facebook

Friday 13 November 2015

Serikali yasimamisha wafanyakazi 4 kwa tuhuma za wizi wa kuaminika Kilimanjaro.

Wafanyakazi wanne wa halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamesimamishwa kazi na mweka hazina wa hospitali ya machame amefukuzwa kazi kwa tuhuma mbili tofauti za wizi wa kuaminika wa kujipatia zaidi ya shs.74mil/=.

Mkuu wa wilaya hiyo Bw Antony Mtaka amesema, wafanyakazi wawili wa idara ya fedha Valentine Elisha na Edwin Kalokora wamehusika kugawana shs. 38mil/=kwa ushirikiano na mweka hazina huyo Philipo Masasi ambazo zilikuwa posho ya kujikimu madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo. 

Bw Mtaka amewaambia wafanyakazi wa hospitali hiyo ya KKKT kuwa, wafanyakazi wawili wa idara ya utumishi Faraja Ndatu na Isaya Bahege  walighushi nyaraka za serikali zikiwemo nembo za halmashauri na saini za madaktari waliofariki na kustaafu na kuchukua mkopo wa shs. 36mil/= kutoka benki ya CRDB. 
Mkurugenzi wa hospitali ya Machame Dr Laiser Saitore amesema, fedha hizo ziliidhinishwa kisheria na wahusika wote kati ya Nov 2014 hadi Feb mwaka huu lakini hazijafika katika hospitali hiyo hadi sasa. 

Mganga mkuu wa wilaya ya Hai Dr Paul Chaote amesema, ufisadi wa fedha hizo waliugundua baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Saitore kutokana na kutowasili kwa fedha hizo kwa miezi nane. 

0 comments:

Post a Comment