Facebook

Friday 13 November 2015

Kikwete afurahia kasi ya Rais Magufuli.

Rais aliyeondoka mamlakani majuzi nchi Tanzania amesifu jinsi Rais mpya John Magufuli ameanza kufanya kazi na kumtaka aendelee vivyo hivyo.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete alisema hayo wakati wa kukabidhi rasmi ofisi yake kwa Rais Magufuli aliyeapishwa Novemba 5 baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25.

“Umeanza vizuri, baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi,” alisema Bw Kikwete.

Dkt Magufuli amekuwa akifanya ziara za kushtukiza, ya kwanza ikiwa katika makao makuu ya Wizara ya Fedha siku yake ya kwanza kazini ambako aliwakuta wafanyakazi wengi wakiwa wametoka ofisini.

Siku chache baadaye, alifanya ziara ya kushtukiza hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alisikitishwa na utoaji huduma.Hafla ya kukabidhi rasmi afisi kwa Rais Magufuli ilishuhudiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Maafisa wa Ofisi Binafsi ya Rais.

Magufuli alisikitishwa na utoaji huduma Muhimbili na akabadilisha usimamizi wa hospitali hiyoKwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu, Rais mstaafu Kikwete alimkabidhi Rais Magufuli taarifa rasmi yenye kurasa 53, ambayo kwa ujumla inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika, ambazo zinasubiri kukamilika na zile ambazo zinasubiri maamuzi ya utekelezaji.Mengine ni hali halisi ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

0 comments:

Post a Comment