Facebook

Wednesday, 11 November 2015

Rais wa Nigeria amfuta kazi mkuu wa Taasisi ya kupambana na rushwa na kumteua Mwingine.

Siku moja baada ya rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kumfuta kazi mkuu wa taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo Economic and Financial Crimes Commission (EFCC).

Kamishna wa polisi bwana Ibrahim Mustafa Magu ndiye ameteuliwa kuiongoza EFCC kama kaimu mkuu.Msemaji wa rais Buhari, Garba Shehu, amesema kuwa kamishna wa polisi bwana Mustafa Magu atachukua usukani katika taasisi hiyo ya kupambana dhidi ya rushwa.

Hakuna sababu zilizotolewa kwa kumpiga kalamu Ibrahim Lamorde,ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu 2011.Hata hivyo Mwezi Agosti, Lamorde alikanusha madai kuwa takriban dola bilioni 5 zilikuwa zimetoweka katika akaunti za benki za tume hiyo.Wakati huo bwana Lamorde alisema wanaoeneza uvumi huo walikuwa wanamtupia tope tu kwani haikuwa ukweli.

Rais Buhari anataka kuhakikisha kwamba mawaziri wapya atakao wateua hawatatumia ofisi kujinufaisha.Baraza lake la mawaziri linatarajiwa kuapishwa baadaye wiki hii, zaidi ya miezi tano baada ya kuingia madarakani.Image captionLamorde alisema wanaoeneza uvumi huo walikuwa wanamtupia tope tu kwani haikuwa ukweli.

Rais Buhari alishinda kiti cha urais mwezi Machi, katika uchaguzi mkuu wa kihistoria na akaahidi kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma.

Rais Buhari anadhaniwa kuwa na mitazamo ya kiimla ikija kwa maswala ya kupambana na ufisadi uliokithiri nchii humo na hivyo inadaiwa kuwa amechelewa kuapisha baraza lake la mawaziri kwa zaidi ya miezi 5 ilikupiga msasa kikamilifu mawaziri wake.

Rais huyo anaamini kuwa ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi ndio unaoizuia nigeria kunawiri ipasavyo licha ya kuwa na uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

Related Posts:

  • Kiongozi ataka vijana wajihami Nigeria Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mingi Kiongozi mmoja wa kijamii katika mji wa Chibok Nchini Nigeria ameiomba serikali ya taifa hilo kuwaruhusu kubuni makundi ya vijana waliojiham… Read More
  • Mashoga wapinga Urais wa Kutesa UN Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa. Uwezekano wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa, kushinda cheo cha Urais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kumeanzisha mjadala mkali nchini Uganda,… Read More
  • Atafuna Moyo wa binadamu Afrika Kusini..   Mtuhumiwa alipatikana akila moyo wa binadamu kwa kisu na uma Polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza t… Read More
  • Obama:Iraq inahitaji msaada. Rais wa Marekani Barack Obama amesema serikali yake inatazama "njia mbalimbali" ikiwemo nguvu za kijeshi kuisaidia Iraq kupambana na wanamgambo. Obama amesema Marekani ina nia ya kuhakikisha wapiganaji hawachukui tena… Read More
  • Mhubiri mwingine auawa nchini Kenya Marehemu Sheikh Mohammed Idris ameuawa na watu wasiojulikana Hali ya ulinzi imeimarishwa mjini mombasa kufuatia kuuwawa kwa Muhubiri mmoja wa kiisilamu m… Read More

0 comments:

Post a Comment