Facebook

Friday 13 November 2015

Klabu ya Lille yawasilisha rasmi ofa ya kumsajili Samatta.

Klabu ya Lille inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa imewasilisha rasmi ofa ya kumsajili mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC) na Taifa Stars, imefahamika.

Katika mahojiano na moja ya vituo vya televisheni vya Afrika Kusini usiku wa kuamkia jana, Mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi, alisema klabu hiyo imewasilisha maombi hayo na sasa wanasubiri kuitwa kwa ajili ya kufanya mazungumzo.

Katumbi alisema Lille ndiyo klabu ambayo imekuwa ikikumbushia maombi yake mara kwa mara tofauti na klabu nyingine zilizowasilisha maombi ya kumnasa straika huyo ambazo hata hivyo, hakuwa tayari kuzitaja.

Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo, pia alikiri kufahamishwa juu ya ofa ya Lille na kueleza kuwa waliamua kusimamisha mazungumzo kuzipa kipaumbele mechi mbili za fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya USM Algiers ambazo TP Mazembe walishinda zote na kutwaa ubingwa.

"Hiyo ofa ninaijua, ilikuwa mapema na tulikubaliana mjadala wake uanze baada ya mechi za fainali kumalizika, wakati wowote tunaweza kukutana nao kwa ajili ya kuijadili," alisema meneja huyo.

Kisongo aliongeza kuwa hawatakuwa na papara katika kufanya uamuzi kwa sababu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yuko katika kiwango cha hali ya juu kwa sasa.

Alipotafutwa na mtandao huu wa
Bantuz jana kuzungumzia masuala ya usajili, Samatta alisema atakuwa tayari kuanza kuzungumzia mahali anapokwenda baada ya kuitumikia nchi (Taifa Stars) katika mechi mbili zinazoikabili dhidi ya Algeria.

0 comments:

Post a Comment