Facebook

Sunday 15 November 2015

Na Happiness Katabazi:- DK.TULIA ACKSON HUFAI KUENDELEA KUWA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

NAIBU Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,Dk.Tulia Ackson  Novemba 11 Mwaka huu, amechukua fomu ya Kugombea nafasi ya Spika kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Ieleweke kwamba Cheo cha Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ni Cheo Che kiutendaji na hivyo anayeshikilia Cheo hicho ni mtumishi wa Umma kwa maana Kuwa ni Wakili wa Serikali ambaye Sheria ya Utumishi wa Umma ha imruhusu Kuwa mwanasiasa wala kujiunga na vyama vya Vya siasa.

Lakini Dk.Tulia amejidhihirisha wazi Kuwa licha ni mtumishi wa umma mwenye Cheo cha juu serikali ni mwanasiasa wa CCM. Na Watendaji wa idara za Utoaji wa Haki kama Wanasheria wa serikali, Mahakimu na Majaji hawapaswi Kuwa wanasiasa wala kujiunga na vyama Vya siasa kwa Sababu ya kukwepa kukosa  kuaminiwa na umma Kuwa hawawezi Kutenda haki .

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk.Tulia alipoenda kuchukua fomu ya Uspika mapema wiki hii ametudhihirishia yeye ni mwanasiasa na wakati huo huo ni mtumishi wa umma .

Ni wazi hafai kuendelea kushika Cheo hicho endapo akikosa Uspika kwasababu Tayari Utendaji wake umeanza kutiliwa Mashaka Kuwa hawezi Kutenda Haki kwa wananchi ambao  siyo wana CCM na ukweli ni kwamba amepoteza ' Public Confidence'.

Ibara ya 21(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inatoa haki kwa wananchi wake ya kuchagua, kuchaguliwa,au kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala".

Hivyo  Dk. Ackson  ambaye ni miongoni mwa wagombea Nafasi ya Uspika kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) , Ana Haki hiyo ya Kikatiba ya Kugombea nafasi hiyo ya Uspika licha ni Mtumishi wa serikali tena Mwandamizi.

Itakumbukwa Kuwa Septemba 9 Mwaka huu, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alimteua Dk, Ackson Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo ambao anaushikiria hadi sasa alikuwa ni Mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.

Dk.Ackson  kwa sasa siyo Mbunge ila anagombea nafasi ya Spika kwasababu Ibara ya   84(1) ya Katiba ya nchi inatoa haki kwa mwananchi kugombea nafasi hiyo ya uspika hata kama siyo Mbunge na inasomeka hivi ;

"  Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge."..

Nimelazimika kuandika makala hii Leo kwasababu uamuzi wa Dk.Ackson Kugombea nafasi ya Uspika wakati akiwa na wadhifa wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye Moja ya jukumu la Mwanasheria Mkuu wa serikali kuishauri serikali Katika masuala yote ya Sheria.

Kwanza napenda kumpongeza Dk.Ackson kwa kuteuliwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali mwanamke mwanamke wa kwanza Tanzania tena mwenye  umri Mdogo .Hongera sana .

Pili nampongeza kwa ujasiri wake wa kuamua kujianika hadharani bila kujali madaraka makubwa aliyonayo wala miiko ya Kazi yake ya Mwanasheria wa Serikali  Kuwa yeye ni Mwanachama wa CCM  na mwanasiasa.

Tatu nampongeza Dk.Acksonkwa uwazi  wake wa kuamua Kugombea nafasi ya Uspika ikiwa ni siku Chache tu tangu alipoteuliwa Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9 Mwaka huu. Hatari sana.

Nne, Nampongeza sana Dk.Ackson  kwa kuchukua fomu ya Uspika kwasababu ni wazi sasa umedhiirishia umma Kuwa hiyo Nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,haitaki  na Cheo hicho ni kidogo sana kwake hivyo unataka Cheo kingine kikubwa Uspika.Yangu  macho.

Tuelezane ukweli ,licha Dk.Ackson  Ana Haki ya Kugombea nafasi hiyo nanina mgombea     ashinde licha kwa asilimia 99 hawezi kushinda nafasi ya Spika .Na ikitokea Akakosa hiyo nafasi umma hasa vyama Vya upinzani  utamwamini tena Katika Utendaji wake?

Maana siyo Siri Dk.Ackson  alipoenda kuchukua fomu Tayari Yale maneno yaliyokuwa yakisemwa na wapinzani Kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ina baadhi ya Wanasheria wa serikali wanatumiwa na CCM kwa   maslahi ya CCM licha wapinzani Hao hawakuwahi kutoa vielelezo vinavyoonyesha ni Mwanasheria yupi wa serikali ni Mwana CCM.

Lakini kupitia Mgombea Uspika ambaye ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali  sasa wapinzani wamepata ushahidi Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye ni mtumishi Mwandamizi wa serikali  Mwana CCM na uthibitisho ni kwamba ametumia Kadi yake ya uaachama wa CCM kwenda Kugombea nafasi ya Uspika.

Hivyo ni wazi sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivi sasa imebaki Ukitazamwa ndivyo sivyo kwasababu ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda Kugombea nafasi ya Uspika kwa tiketi ya CCM .

Kama hivyo ndivyo, huyu Dk.Ackson  uchaguzi wa Spika ukimalizika na ikatokea akashindwa hivi akirudi ofisini kwake wananchi tutakuwa tunamtazamaje zaidi ya kubaki na hisia na maswali dhidi yake Kuwa hawezi Kutenda Haki sawa kwa wote kwasababu Tayari ameishaonyesha yeye ni Mwanachama wa CCM wakati hapaswi Kuwa mwanasiasa ?

Uchaguzi Mkuu umekwisha ,Kesi za kupinga Matokeo ya Ubunge lazima zitafunguliwa Katika baadhi ya Mahakama zetu na Kesi hizo mdaiwa wa kwanza ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mbunge aliyeshinda na Msimamizi Wa uchaguzi.

Enzi zake Mwanasheria Mkuu wa sasa George Masaju akiwa na wadhifa wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa akienda Mahakamani Mwenyewe kuiwakilisha serikali pindi iliposhitakiwa au serikali ilipofungua Kesi dhidi ya mtu,au Taasisi Fulani.

Hata sasa hivi Mwanasheria Mkuu wa serikali hazuiwi kwenda mahakamani kuendesha baadhi ya Kesi ila kutokana na jukumu zito anaamua  kukasimu majukumu Mawakili wa serikali na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Na Mfano hai ni Oktoba Mwaka huu, Kada wa Chadema alifungua  Kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam itoe Tafsiri ya mita 200 Katika Kesi maarufu ya mita 200 .

Masaju alimtwisha jukumu hiyo Naibu wake Dk.Tulia na Wanasheria wengine wa serikali kwenda kutetea Kesi hiyo hiyo na hatimaye walishinda.

Swali langu Je , itokee siku aliyekuwa mgombea Ubunge wa vyama Vya upinzani Kufungua Kesi ya kupinga Ubunge wa Mbunge wa CCM halafu Dk.Ackson  aende kuitetea hiyo Kesi mahakamani.

Je Yule mlalamikaji ambaye alikuwa mgombea toka vyama Vya upinzani akiiambia  Mahakama Kuwa Hana Imani na Dk.Ackson  Katika Kesi hiyo kwasababu ni Kada wa CCM na hivyo hatoweza kusaidia Mahakama Kutenda Haki Atakuwa amekosea?

Sina Chuki na Dk.Ackson  na sina Sababu ya Kujenga Chuki naye ,ila tu napenda kumweleza kijana mwenzangu Kuwa Kabla ya kuchukua uamuzi aliouchukua wa Kugombea Uspika akijitafakari kwanza yeye kwasasa ni nani?Ana wadhifa gani?Anafahamu Jamii itamtafsiri vipi?

Je anapoenda Kugombea Uspika awe na uhakika Kuwa atashinda na asiposhinda basi atakuwa amejipunguzia  asilimia za kutoaminiwa Katika suala zima za Utoaji Haki hasa Katika vyombo vyetu Vya Sheria hata kama Atakuwa anatenda Haki kweli kwasababu Tayari ameishauthibitishia umma yeye ni Mwanachama wa Chama Fulani.

Hivi Leo hii itokee Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mgonjwa au amesafiri nje ya nchi au amefariki ghafla na hivyo kusababisha Naibu Mwanasheria wa Serikali Dk.Tulia kukaimu Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ,awe Bungeni anatoa ushauri wa kisheria ndani ya Bunge kuhusu muswaada Fulani au jambo Fulani ambalo wabunge wa upinzani hawalitaki hata kama ni kweli Dk.Tulia yupo sahihi kisheria, wale Wabunge wa upinzani wakiamua kumpinga kwa Kigezo yeye anatetea huo muswaada kwasababu pia ni Mwanachama wa CCM, at akasirika au sisi wananchi na viongozi wa serikali hiyo Hali watachukuliaje?

Kwa mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya nchi inasema Mwanasheria Mkuu atakuwa Mbunge kutokana na wadhifa .

Ibara hiyo haijasema Mwanasheria Mkuu wa serikali atakuwa mbunge  
wa Chama Fulani cha siasa.

Ieleweke kwamba uteuzi wa Dk.Ackson  ulizua  minong'ono na maswali mengi chini kwa chini kutoka Katika Kada ya Wanasheria hasa wa serikali licha ana elimu nzuri licha tu hajawahi Kuwa Wakili wa serikali na Hana udhoefu wa uendeshaji wa Mashitaka.

Baadhi ya watu wa Kada ya Sheria Walisema licha Rais anayo mamlaka ya Kumteua mtu yoyote kushika wadhifa wowote ,Walisema aikuwa busara kwa  Rais Kikwete   kuacha kuteua Mawakili wa serikali kushika Nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwenda kumteua Dk.Ackson  ambaye hata miiko ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali hajaijua .

Kumbe sasa wale waliokuwa wakipata Mashaka kuhusu Utendaji wa Dk.Ackson kwa upande Fulani sasa tunaweza Kusema walikuwa sahihi kwasababu kitendo cha Dk.Ackson Kugombea nafasi ya Uspika wakati yeye ni mtumishi wa umma na hapaswi Kuwa mwanasiasa tena katika kipindi kifupi tu ni dhahiri sasa miiko ya Kazi yake haifahamu na hakutaka kuifahamu  akaamua kukurupuka na kufanya hicho alichokifanya ambacho kimesababisha watu kutulia mashaka utendaji wake.Aibu sana.

Kuna taarifa zisizo rasmi Kuwa Dk.Ackson ametumwa kwa makusudi na kiongozi mmoja Mwanamke ambaye ni Waziri na ana nafasi kubwa ndani ya CCM agombee nafasi hiyo   ili aende kuwaganya kura za baadhi ya wagombea Uspika ambao ni tisho kwa hao waliomtuma Dk.Ackson.

Kwa Kuwa sina ushahidi na taarifa hizo Mimi nitabaki kuamini Dk.Ackson amegombea Uspika bila kutumwa na mtu.

Ila taarifa hizo   ziwe za kweli  au siyo za uzushi, zinazidi kujengea Mashaka Utendaji wa  Dk.Ackson kutokana na Cheo Chake na yote hayo yanampata na yatazidi  kumpata kwasababu ameamua kuingia Kwenye siasa ,asingeingia huko yasingemfika.

Hakuna ubishi Kuwa Dk.Ackson  kwa kitendo chake cha kugombea uspika licha ana haki ya Kikatiba kugombea, amedhihirisha kuwa yeye ana papara ya kupata madaraka makubwa tena kwa vipindi vifupivifupi ili Hali bado Ana umri Mdogo.

Ushahidi ni huu Septemba 9 kateuliwa na Rais Mstaafu Kikwete kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Novemba 11 Mwaka huu, kachukua fomu ya Kugombea Uspika.

Hivi tukisema Dk.Ackson  ameudharau,aupendi na autaki uteuzi  Rais Kikwete wa alipomteua yeye Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali tutakuwa Tunakosea?

Maana Aiingii akilini kwa Kipindi kifupi hicho alichoteuliwa kushika nafasi hiyo nzito serikali halafu aamue kwenda kuwania nafasi ya Uspika halafu tuache kuamini kuwa Dk.Ackson  ile nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaipenda?

Aipendi na ninatabiri anaweza asidumu Katika wadhifa huo kwa muda mrefu kwasababu Tayari ameishaonyesha wazi Ana tamaa ya kupata madaraka makubwa kwa harakahara na hataki kujifunza Kazi kutoka Kwa waiomtangulia na akae akijua baadhi ya watendaji wake wa chini wamekerwa na yeye kiongozi wao kujiingiza Kwenye siasa wakati haruhusiwi Kuwa Mwanachama wa Chama cha siasa.

Hivi wewe Dk.Ackson  kama umegombea Uspika sasa ,nikuulize Je umepata muda saa ngapi ya kukaa na Mawakili wa serikali wakawa wana kufundisha jinsi ya kuendesha hiyo Ofisi na wewe ukapata uzoefu ?

Ni wazi bado unaitaji kupikwa na Wanasheria wa serikali ili uive  lakini ni wazi sasa umeonyesha hata huo muda wa kukaa kitako upikwe na watangulizi wako katika hiyo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali huna unawaza Kugombea madaraka ya kisiasa.Huzuni.

Minakushauri, kuliko kuendelea kushikilia nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali wakati matamanio yako ni Kugombea Uspika na siasa, ni vyema ungeandika barua ya kujihudhuru wadhifa huo mapema ili Rais mpya Dk.John Magufuli ateue mtu mwingine ambaye kwanza ana uzoefu na kazi ya wakili wa serikali ambaye akili zake zimetulia,maana wewe bado hujatulia ili afanyekazi.

Wewe Dk,Ackson tayari  umeishaonekana mguu mmoja upo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mguu mwingine upo CCM Kugombea madaraka makubwa ya kisiasa.

Sasa mtu wa aina ya Dk. Tulia ni wazi Utendaji wake katika madaraka aliyonayo hautakuwa mzuri maana muda mwingi atakuwa fikra za kupanga mikakati ya jinsi ya kupata nafasi nyingine kubwa zaidi ya hiyo tena kwa chap chap.

Dk.Tulia unapaswa utambue jambo Moja Kuwa wanasiasa siyo watu wa kuaminika sana.Wakikupa ushauri wa kufanya jambo lolote hata hili la Kugombea Uspika ulitakiwa ulitafakari sana kwamba endapo ukikosa nafasi hiyo wewe hadhi yako Mbele ya Jamii inakuwaje.

Umeanza kutiliwa Mashaka na baadhi ya Jamii,lakini waliokushauri  ugombee Uspika hawatakusaidia kuminya fikra za watu na baadhi ya watendaji wako wasikuone wewe ufahai tena kuendelea Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa kitendo Chako cha Kugombea Uspika kupitia CCM licha siyo kosa la jinai.

Niitimishe kwa Kusema Kuwa Dk.Ackson endapo ukikosa nafasi ya Spika ,hufai kuendelea Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwasababu Tayari umeonyesha wewe ni mwanasiasa hivyo Utendaji wako unatiliwa Mashaka.

Pia nakushauri acha pupa ya kuwania  madaraka ili Hali wewe ni msomi na bado ni binti Mdogo sana licha una elimu kubwa lakini bado unaitaji kuelewa,kupikwa na waliokutangulia na wenye uzoefu Katika eneo la Mawakili wa Serikali ,siasa utafanikiwa.

Au kama fikra na moyo wako hautaki uendelee Kuwa na  Cheo cha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,zinakutuma kwenda kufanya siasa ni vyema basi ukaomba Kibali cha kumuona Rais Magufuli ili umeombe akutoe Katika Cheo hicho au wewe Mwenyewe andika barua ujiudhuru kuliko kufanya hili uliofanya  ambalo linakatazwa kabisa Kuwa Mwanasheria wa serikali Kuwa mwanasiasa lakini wewe mwenzetu bila woga tena hadharani umeonyesha wewe ni mwanasiasa wakati huo huo ni mtumishi wa umma.

Dk.Ackson nakupenda ebu punguza kasi kidogo ya matamanio ya kupata madaraka inakusaidia Kwani Mtaka yote ukosa yote Waswahili Walisema.Nakutakia kila la kheri Katika mbiyo zako za Uspika.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
14/11/2015

0 comments:

Post a Comment