Facebook

Saturday 17 January 2015

BERAHINO AFUNGIWA KUENDESHA GARI MIEZI 12

Mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino amepigwa marufuku kuendesha gari kwa kipindi cha miezi 12 baada ya kukiri kosa la kuendesha gari akiwa amelewa. Berahino, 21 alikamatwa na polisi saa za alfajiri Oktoba 22 mwaka jana. Mahakama ya mwanzo ya North Cheshire mjini Runcorn pia imempiga faini ya pauni 3,400.
Mchezaji huyo kiwango chake kimekua kiasi cha kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England mwezi Novemba, ingawa hakucheza katika mechi dhidi ya Slovenia na Scotland.
Berahino, mzaliwa wa Burundi na ambaye alihamia Uingereza akiwa mdogo, alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu kuichezea West Brom Disemba 2013.

0 comments:

Post a Comment