Facebook

Friday 16 January 2015

“HUU NDIO MUAROBAINI WA MGOMO WA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DODOMA”



 
Ifike mahali siasa zipigwe marufuku vyuoni.Migomo ni miuri kama itafuata taratibu kuhalalisha migomo hiyo na sio kutumiwa kwa ajili ya kunufaisha watu au kikundi fulani.Kuna siku uongozi wa kwenye taasisi za elimu na elimu ya juu ziwe ni kazi (ajira) maalumu.Haya mambo ya maandamano pamoja ni haki za wanafunzi yanapoteza malengo na kuwatia hasara wengine za maisha.Inauma sana siku kadhaa zimepita kuna wanafunzi kadhaa wamepoteza miasha na wengine wamejeruhiwa.Sasa hivi wazazi wa hawa vijana watafaidika vipi na matunda ya vijana wao waliowasomesha kuanzia walipokuwa wadogo hadi kufikia ngazi ya chuo,taifa linapoteza nguvu kazi, Inauma sana.

Taifa linapoteza vijana kwa mambo ambayo yangeweza kufanywa kwenye harakati za siasa za mtaani. Jamani kuna muda wa kufanya na kuna muda wa kujiandaa kufanya. Tukiwa vyuoni huko tuwe tupo kwenye kujiandaa kufanya, na shule ikiisha ni muda wa kufanya.Najua kuna wengine wameathrika zaidi ya hivi hata kama mwili hawakuumia.Huku Taarifa zilizopo kuna wanafunzi amefariki chuo Kikuu cha Dodoma,matatizo ya pale yanayatatulia kinyume na taratibu,wanaoharibu taratibu hizi ni viongozi wanaosimama kama wawakilishi wa wanafunzi tatizo ni siasa tu,vyama vya siasa vinaharibu utaratibu chuo vyuo hususan Chuo Kikuu cha Dodoma,ambapo umetokea mgomo kwa wanafunzi wanaochukua stashahada katika chuo hiko.

Siungi mkono jeshi la Polisi kuhusika na mauaji ya aina yoyote ile.Ila nawaomba vijana wenzangu mliopo katika vyama vya siasa muyapime maneno na maagizo ya viongozi wenu kwa faida ya taifa hili.Kunu huyu ambaye ni kiongozi pale Chuo Kikuu cha Dodoma anaitwa Mwakibinga.Huyu Mwakibinga  zaidi ya miaka 4 aliyokaa nje ya chuo Kikuu cha Dodoma.Hakika palitulia siku za hivi karibuni amerudishwa Chuoni ameanza tena na kuwa sehemu ya kusababisha mauaji ya mwanafunzi wenzake.

 Aliyekuwa Waziri Mkuu Philipo Mwakibinga

"Academic institution is a place to learn not to practice politics although politics is tought” .Ni  maneno ya mwalimu wangu aliyokuwa ananiambia mara kwa mara nilipokuwa nachukua masomo yangu ya sekondari katita shule ya sekondari ya St.Matthew’s 
Waziri mkuu wa chuo Kikuu cha Dodoma Philipo Mwakibinga huyuhuyu,anatumia chuo kama sehemu ya kujijenga kisiasa, ni mtu ambae hana malengo na taaluma yake,hana nia wala malengo na anaowaongoza bali ni mtu mwenye maslahi binafsi,mgomo uliotokea Chuo kikuu cha Dodoma yeye ndie aliyeupika kwa siku sita na usiku wa saa sita kabla ya mgomo huo kutokea ndipo alipofanya kikao cha mwisho cha maandilizi ya mgomo na madhara yake ndiyo haya,wanafunzi wenzake wamepoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Na alifanikiwa kuwalaghai wanafunzi wa stashahada na kuleta haya yaliyotokea,ni maagizo moja kwa moja kutoka kwa wale anaofanyanao kazi kwa karibu,na mgomo huu ilikuwa ajenda ya kikao chao cha tawi walichokifanya kijijini Ng'ong'ona Jumapili ya tarehe 4.
Siasa kwenye vyuo inapoteza malengo ya vijana wengi sana. TusemenI kweli na tuache mahaba ya vyama vyetu. Sikatai wanafunzi kugoma, wote tumekuwa wanafunzi, ila ifike mahali tutazame njia za kutafuta ufumbuzi wa haya yanayotupelekea kugoma. Sasa hapa kwenye huu mgomo ukifanya upembuzi yakinifu kati ya faida na hasara utagundua hasara ni kubwa kuliko faida.

Miongoni mwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma aliyeumizwa vibaya na Polisi 

Polisi wanaweza kuwa walitumia nguvu zaidi kitu ambacho sidhani kama ni jamnbo zuri katika kutawanya na kutatua matatizo.Ila kwa nini wanafunzi wahamasishwe kufika huko? Africans are incapable of sustaining their protests in two days" Prof. Patrick Lumumba
Lakini kwa upande wa pili,serikali hii iliingia dosari tangu katika uchaguzi wao,waliweka siasa na itikadi zao mbele kuliko lengo kuu la wao kuwafanya kuwa pale,mzizi ni mmoja tu,kuondoa ushabiki na kufuta kabisa uwepo wa maswala ya vyama vyuoni.

Kila mtu anajua maafa na hasara ya maandamano lakini tukubaliane kwamba mifumo yetu pia inachangia sana kuwalazmisha vijana kufanya hivyo.Ufaranza juzi walikuwa na maandamano makubwa, Ukraine mwaka jana wamekuwa na maandamano takriban miezi miwili. Tumeshuhudia migomo na maandamano ya kuondoa tawala mbovu kwenye nchi za kiarabu, Brazil na USA migomo ipo.Lakini nchi ndogo kama Tanzania ambavyo hazitambui maana halisi ya migomi katika mfumo utawala wa kidemokrasia matatizo kama haya yanatokea.

Sidhani kama sakata kama la ESCROW lingetokea kwenye nchi inayojielewa watu wangefyata mikia. Sidhani Kama kweli tunachukia maandamano na migomo tuanze kwanza kukemea na kulaani vyanzo vyake.
Nafikiria kuwa hivi vyeo vya kiserikali vifutwe. Tuwe na mwenyekiti na mlolongo wa viongozi wengine ukifuata ili kuondoa kiburi. Lakini pia wanafunzi wanapaswa kujua wametumwa na jamii vyuoni kuhenyea chakula cha kijiji si chao binafsi na wazazi wao. Vyuoni kuna somo liitwalo ‘Political science’ tunaweza kusoma na kisha kuja kufanyia mafunzo ya vitendo uraiani baada ya masomo ili vyuo viwe mahala patulivu.

Maandamano ni kweli njia ya kupaza sauti ya pamoja lakini hakuna ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kuwa maandamano yameleta tija.Nimetolea mfano mapinduzi ya Waarabu kupitia maandamano na kasha kufanya maoinduzi ‘Arab Spring’ mfano Libya,Tunisa,Misri n.k .Hivi leo hii ni kweli Waarabu wanafurahia maamuzi yao? Libya hivi sasa wako katika kipindindi kigumu zaidi katika historia yao, nchi haina amani ya kweli tangia alipoong’olewa Gadaffi madarakani.
Libya,Brazil,Ufaransa binafsi naamini katika majadiliano zaidi ambayo najua ni suluhu isiyoshindikana wakati Mugabe anatoka porini kusaka Uhuru alikuja kwa Mwl Nyerere kuomba ushauri. 

Yeye alitaka kurudi msituni.Mwl Julius Kambarage Nyerere akamwambia "kaa na wazungu mzungumze, ukirudi porini nawaambia nchi za frontliners wakutose" Mugabe akamuelewa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nguvu ya mazungumzo ya hoja. Wazungu wakataka kumuweka kama Rais huku akiwa na waziri mkuu ambaye ni mzungu hilo nalo akakataa.Akataka Urais wenye mamlaka kamili.Kupitia hili nadtumai unaweza kujifunza ulevi wa madaraka unapoitwa Rais. Uenyekiti kidogo hupunguza hisia za kifalme. Ndicho kinachotokea katika klabu kubwa mbili nchini Simba,Yanga pamoja na shirikisho linalosimamia mpira wa miguu nchini TFF. Umungu mtu.

Lakini tusistajaabu sana hiyo ni hulka ya mwanadamu,wapo ambao hawawezi kujifanya miungu watu! Che guevara baada ya kuleta ukombozi nchini Cuba na kuwa waziri baadae aliachia ngazi na kujivua vyeo vyote alivyonavyo ili akalete ukombozi wa dunia.Hoja yangu kubwa ni kuwa wapo viongozi ambao wataweza kuishi na kutenda kutokana na taratibu za vyuo husika na tunayo mifano ya kutosha.Napenda sana kuwa kama sheria inavyotajwa na wahenga kama msumeno ambao unakata huku na huku.

Katika kulitatua tatizo hili ninatoa mapendezo mbalimbali na miongozo mbalimbali ambayo ikitekelezwa baadhi inaweza kutuletea ufumbuzi sahihi.Migomo hata kama kukiwa na wenyeviti kama hatutafuti ufumbuvi wa matatizo ya wanafunzi ni ngumu sana kuisha.Rais wa Chuo Kikuu cha Dodoma anatoa tamko dhidi ya serikali anapata wapi hii nguvu kuna baaadhi ya mambo nampongeza sana Rais Jakaya Kikwete nadhani yeye ni miongoni mwa viongozi pekee Afrika Mashariki aliyeachia uhuru wa kijieleza popote pale sasa hivi hata madaladala nayo yanagoma,ni juzi tu hapa kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimoja kikubwa nchini Nchi aliadhibiwa kifungo baada ya kuyachambua madhaifu ya Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta na kasha kuyaweka hadharani,nadhani huu uhuru unatumiwa vibaya sana na vyama au watu.Hao wa Chuo Kikuu cha Dodoma ukichunguza kiundani ni siasa tu ndani yake  tatizo ni dogo hao watu waliopewa dhamana ya kushughulikia matatizo ya wanafunzi nadhani hawakufanya kazi yao ipasavyo.

Tuseme ukweli kati ya wanavyuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma na serikali ni nani ameadhirrika zaidi? Ifike mahali tupime maamuzi yetu kama yana afya au la! Hivi kweli wewe mwanafunzi umetoka kijijini huko ambako hata barabara haifiki kuipata barabara kuu ni mtihani!! Familia uliyotoka unaijua vyema maisha yalivyo, leo umebahatika nafasi ya kusoma marejesho yake ni migomo hivi hapa unamkomoa nani? Haya leo hii umepata kilema cha kudumu mzazi wako anao uwezo wa kukutibia ? Haya umefukuzwa unaye wa kututetea? Tuachane na wanasiasa someni mmalize kisha nendeni kwenye ulingo wa siasa kama mnaitaka kweli! 

Hao wanasisa walitulia, wakasoma na si kwamba kulikuwa hakuna matatizo la hasha lakini unaangalia kipaumbele chako !
Wanavyuo wa siku hizi hawashikiki wao kila jambo wanajua nadhani lingekuwepo somo la kujua askari akisema tawanyikeni ukikaidi ujue nini kinafuata zaidi ya virungu na mabomu ya machozi ni mawazo yangu tu. Inauma sana mtoto umemsomesha kwa taabu kubwa mno halafu anakwenda kujiingiza kwenye vitu vya hovyo visivyomjenga! Taarifa rasmi zinasema uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) umeazimia kumfukuza chuo moja kwa moja waziri mkuu wa serikali ya
Waziri Mkuu Bwana Mwakibinga mwanafunzi wa “College of humanities and social sciences” ambaye  aliwahi kusimamishwa chuo kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kuruhusiwa kurudi chuoni na kuendelea na masomo. Mwaka jana baada ya miaka kama 3 alirudishwa chuoni na baadae kuingia tena katika siasa ambapo aliteuliwa kuwa Waziri mkuu wa kitivo hicho. Juzi umeibuka tena na mgomo.

Akiwa raisi aliruhusu mgomo wa college yake baada ya wizara ya elimu kutoa maelekezo ya namna watavyoshughulikia suala la field utaratibu ambao yy na serikali yake hawakukubali. Nakumbuka makamu mkuu wa chuo alikuja saa sita usiku kuwasihi wanafunz waendelee na masomo na walifanya mazungumzo na uongozi wa chuo lakini serikali ya wanafunzi hawakusitisha mgomo.
Siasa inavuruga sana vyuo nchini.Lakini serikali nayo inatengeneza bomu linalowalipukia wao wenyewe.Hawa wanafunzi walioko vyuoni wengi wao hawana mikopo mwisho wa siku inapelekea wanafunzi waishi maisha magumu sana huku wengine hususani wabinti inafikia hatua wanajiuza miili you waweze kupata pesa ambayo itawasaidia wajikimu na kuendelea na masomo.

Binafsi naamini njia pekee au ‘muarobaini’ wa matatizo makubwa katika vyuo vyetu ni kuhakikisha serikali inawapa mikopo wanafunzi mbalimbali.Serikali inaweza ikadhibiti mianya iliyopo inayosababisha ubadhilifu mkubwa wa fedha na kusimamia vilivyo sekta mbalimbali zinazoliingizia taifa kipato hususani kodi na vyanzo vingine mbalimbali ili ipate uwezo wa kuwahudumia wanafunzi wote waliopo vyuoni na kuacha kutengeneza matabaka kwa kuwapa baadhi mikopo na kuwanyima wengine ili hali hawana uwezo wa kuendesha maisha yao ya vyuo nchini.

Nawasilisha hoja……………………………………………………………………

Imeandaliwa na...............
                                         Katemi Methsela

0 comments:

Post a Comment