Facebook

Saturday 17 January 2015

WANYAMA NJE KWA WIKI TANO

WANYAMA NJE KWA WIKI TANO
Kocha wa Southampton, Ronald Koeman ana wasiwasi kuwa huenda Victor Wanyama akakosa kucheza kwa hadi wiki tano baada ya kuumia msuli wa paja katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Ipswich.
Wanyama alitolewa muda mfupi kabla ya mapumziko, katika mechi ambayo Southampton walishinda 1-0.
Koeman, ambaye amesema mechi za marudiano, katika kipindi hiki chenye mechi nyingi ni "wazimu", alikuwa amepanga kumchezesha Wanyama kwa dakika 45 tu.
"Tuna majeruhi wengine tayari. Kama ni msuli wa paja, basi itakuwa wiki nne au tano." amesema Koeman.
Wanyama, ambaye ni mchezaji wa kimataifa kutoka Kenya amekuwa mchezaji muhimu kwa Southampton msimu huu, akicheza mechi 24.

0 comments:

Post a Comment