Facebook

Saturday 17 January 2015

VAN GAAL:FALCAO LAZIMA AJITUME

 FALCAO LAZIMA AJITUME: VAN GAAL
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema mshambuliaji Radamel Falcao lazima athibitishe uwezo wake ili kupata namba Old Trafford. Falcao, 28, amefunga mabao matatu tangu alipojiunga na Man Utd kwa mkopo wa pauni milioni 6 kutoka Monaco. Van Gaal amesema: "Kama mchezaji ana thamani ya pauni milioni 95 au elfu tano, hakuna tofauti, lazima uoneshe uwezo wako."
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Colombia, hakuchezeshwa kwenye mechi dhidi ya Southampton Jumapili iliyopita Utd walipochapwa 1-0.
Ameanza mechi saba za ligi kuu, na wakala wake Jorge Mendes amesema huenda Falcao asiongeze mkataba wake.
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema mshambuliaji Radamel Falcao lazima athibitishe uwezo wake ili kupata namba Old Trafford. Falcao, 28, amefunga mabao matatu tangu alipojiunga na Man Utd kwa mkopo wa pauni milioni 6 kutoka Monaco.

 Van Gaal amesema: "Kama mchezaji ana thamani ya pauni milioni 95 au elfu tano, hakuna tofauti, lazima uoneshe uwezo wako."
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Colombia, hakuchezeshwa kwenye mechi dhidi ya Southampton Jumapili iliyopita Utd walipochapwa 1-0.
Ameanza mechi saba za ligi kuu, na wakala wake Jorge Mendes amesema huenda Falcao asiongeze mkataba wake.

0 comments:

Post a Comment