Facebook

Saturday 31 January 2015

Apple yavunja rekodi kwa uuzaji wa vifaa vyake duniani.

Kampuni ya kutengeza vifaa vya elektroniki, Apple, imetangaza kupata faida ya dola bilioni 18.8 katika kipindi cha miezi minne ya mwisho mwaka jana , na kuifanya kuwa kampuni ya umma iliyopata faida kubwa zaidi duniani.
Apple bila shaka imeipiku,ExxonMobil iliyopata faida ya dola bilioni 15.9 mwaka 2012 kulingana na ripoti ya kampuni ya Standard and Poor's.

Inaarifiwa hii ndio faida kubwa zaidi katika historia ya kampuni hio kuwahi kushuhudiwa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, mdadaisi mkuu wa kiuchumi wa kampuni hio, Tim Cook alisema kuwa hitaji la simu za iphone duniani ni kubwa kupindukia.
Hata hivyo, alisema kwamba hitaji la tabiti au iPad haliko juu kama ilivyotarajiwa na liliendelea kushuka kwa asilimia 18 mwaka 2014 ikifananishwa na mwaka 2013.

Kadhalika hitaji la simu ya iPhone 6 Plus lilionekana kuwa chachu katika faida za kampuni hio.
Hata hivyo, Apple haikufafanua mauzo ya simu ya iPhone 6 na simu nyinginezo.
Hisa za kampuni ya Apple zilipanda kwa asilimia 5 baada ya soko la hisa Marekani kufungwa Jumanne.
Mmoja wa wanaofuatilia mauzo ya bidhaa za Apple sokoni, na mhariri wa mtandao wa "Cult of Mac" alisema kwamba mauzo ya iPhone yamekuwa juu sana ikilinganishwa na matarajio.

0 comments:

Post a Comment